Na Daud Magesa,TimesMajira Online
JESHI la Polisi linachunguza kifo cha mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ye Sekondari Morning Star,Fatuma Makaranga mkazi wa Mtaa wa Ndofe wilayani Nyamagana.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 mwili wake unadaiwa kukutwa ndani ya tenki la maji nyumbani kwao baada ya kutoweka kwa siku kadhaa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha tukio la kifo cha mwanafunzi huyo na kwamba kabla ya kufikwa na mauti alitoweka nyumbani kwao Mei 25, mwaka huu na kutafutwa bila mafanikio.
Amesema, marehemu huyo alitoweka nyumbani baada ya kutokea mtafaruku kati yake na baba yake ambapo mwili wake uligunduka Juni 4, mwaka huu, majira ya saa 5:51 usiku katika Mtaa wa Ndofe wilayani Nyamagana,ukiwa kwenye Simtanki la maji nyumbani kwao.
Amesema kuwa, jeshi hilo linafanya uchunguzi wa tukio la kifo cha mwanafunzi ili kufahamu mazingira na chanzo chake ingawa hakuna mtu anashikiliwa hadi sasa.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani