Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Dar
MWANAFUNZI wa Shahada ya Sayansi ya Uzamili na Mipango na Menejimenti ya kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Morogoro Nelson Kisanga amebuni mradi wa mfumo unaojumuisha ufungaji wa samaki na kilimo cha mbogamboga.
Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimatafa DITF yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam Nelson amesema mfumo huo unamuwezesha mtu kufanya kilimo na ufugaji kama njia ya kujiajiri mwenyewe.
Amesema mfumo huo unajumuisha ufungaji samaki na kilimo kwa pamoja lengo likiwa ni kukabiliana na chagamoto ya ajira.
“Tumekuwa tukibuni miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ufungaji samaki pamoja na kilimo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza mtu kuweza kujiajiri mwenyewe badala ya kusubiri kuajiliwa”amesema
Kisanga amesema miradi hiyo wamekuwa wakiibuni chini ya kituo cha Uwatamizi na Malezi ya vijana chuoni hapo ambapo wanafunzi upata Mafunzo ya bunifu mbalimbali.
Vilevile amesema mradi wingine wanaoufanya chini ya kituo hicho ni pamoja na kubadili taka taka na kuwa wadudu kwa ajili ya chakula cha mifugo kama vile kuku, Nguruwe na hata samaki.
“Tunafanya vitu vingi pia kituo hiki kimetusaidia vijana kufika mbali kwani tayari tumeshasajili kampuni yetu ya Real Agriculture Group,” amesema Kisanga.
Ameongeza kuwa kupitia kituo hicho wameweza kuongeza mnyororo wa thamani kwa kukuchakata viazi lishe na kupata unga kwa ajili ya kutengeneza juisi, chapati na mikate.
Kisanga amesema chuo Kikuu cha Mzumbe kimekuwa kikitayarisha vijana kuona fursa mbambali za kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Morogoro Dkt. Bahati Ilembo (PHD), amesema chuo cha Mzumbe kinatoa programu nyingi za ujasiriamali na kwamba kituo cha Uwatamizi kinahusika kukuza vipaji vya vijana.
” Tunakuza vipaji vyao kwa kukusanya mawazo yao na ubunifu wanapokuwa katika kituo hiki wanajengwa na kuongezwa uwezo ili mawazo yao ya ubunifu yaweze kuwasaidia,” amesema.
Awali Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka chuo hicho Rose Joseph amesema katika Chuo hicho wamekuwa wakifanya miradi mbalimbali sambamba na kutoa ushauri kwa watu wanaofanya biashara.
“Katika kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita katika kuinua uchumi na kufikia wa kati Chuo Kikuu cha Mzumbe kimekuwa kikibuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kukuwezesha kijana kujiajiri pindi anapomaliza masomo yake”amesema
Aidha alitoa wito kwa watanzania kutembelea Chuo hicho katika Maonyesho hayo ili waweze kujifunza na kupata ushauri wa masuala mbalimbali.
More Stories
CP.Wakulyamba ashuka Katavi na Nguzo nne za Uongozi
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto