Na Moses Ng’wat, TimesMajira Online, Songwe
POLISI Mkoani Songwe wanamtafuta mwalimu Tunu Brown (37) wa shule ya msingi Senjele, Wilaya ya Mbozi kwa6 tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake wa darasa la sita (jina limehifadhiwa) kisha kutoroka.
Kamanda wa polisi Mkoa6 wa Songwe, Theopista Mallya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa lilitokea Aprili 17,2023 majira ya saa 4:45 asubuhi.
Alisema mwalimu huyo ambaye kwa sasa ametoroka alitumia mbinu ya kumlaghai mwanafunzi huyo kuwa atakuwa akimsaidia kwa mambo mbalimbali.
“Tunaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyu (mwalimu Tunu) ambaye alitoroka muda mfupi baada ya kufikishwa ofisi za kijiji na walimu wenzake ambao ndio walibaini kuwa mwenzao kafanya tukio hilo” alifafanua Kamanda Mallya.
Akizungumzia mkasa uliomkumbwa Mwanafunzi huyo ambaye jina lake limegifadhiwa kwa sababu za kisheria amesema siku ya tukio mtuhumiwa (mwalim Tunu) alimuita nyumbani kwake na kumkaribisha ndani.
“Nilipoingia ndani alinipa kiti na kuniambia unataka nikusaidie kitu gani…lakini mimi nilimwambia sihitaji msaada wowote ndipo akanivutia chumbani na kuanza kunibaka” Alisimulia mwanafunzi huyo.
Tukio hilo limeibua hisia kali baada ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Abdalah Nandonde na Tume ya utumishi wa walimu (TSC ) Mkoa wa songwe kuchukua hatua kali kwa walimu ambao wabashindwa kusimamia maadili ya utumishi wa umma.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini