Na Ashura Jumapili,TimesMajira online Kagera ,
Jeshi la Polisi mkoani Kagera,limethibitisha kukamata Mwalimu wa Taaluma shule ya msingi Rulanda, Kata ya Rulanda wilayani Muleba mkoani Kagera,Lameck Jonasambaye anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake muhitimu wa darasa la saba mwaka huu mwenye umri wa miaka 13.
Akiongea kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoani humo Blasius Chatanda,amesema mtuhumiwa ametafutwa na amepatikana anashikiliwa na polisi.
Kamanda Chatanda,anasema taratibu nyingine za kisheria zinaendelea na muda wowote atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Ikumbukwe kuwa, taarifa ya tukio hilo, liliibuliwa Novemba 4,2024 na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Kagera,ambayo walifunga safari na kutoka Bukoba Mjini hadi wilayani Muleba,na kufanikiwa kuzungumza na mtoto huyo pamoja na wazazi wake.
Ambapo tukio hilo lilitokea Oktoba 30, mwaka huu majira ya jioni baada ya mtoto huyo akiwa na wanafunzi wenzake kufika shuleni hapo majira ya mchana kwa ajili ya kuomba mwalimu huyo awaangalizie matokeo ya mtihani wa darasa la saba.Ndipo mwalimu huyo alimwambia binti huyo kuwa ameshindwa mtihani hivyo arudi baadaye ili ampe ushauri.
“Nilirudi nyumbani nikawambia wazazi kuwa nimeambiwa na mwalimu nimeshindwa mtihani hivyo nirudi shuleni saa 10:00 jioni anishauri, ulipokaribia huo muda wazazi waliniruhusu nilirudi shuleni nimsikilize mwalimu Jonas, niliporudi nilimkuta ofisini akaniambia niende darasani tulikokuwa tunasomea atanikuta “anasema mtoto huyo.
“Nilimsubili darasani na baada ya muda alifika akaanza kufunga madirisha na mlango, alipomaliza akaniambia nivue nguo nikakataa, akanifungua zipu akaanza kunipaka dawa kwenye shingo, matiti, kwapani na kwenye kitovu.Akatoa nyingine akanipaka mgongoni alipomaliza akachukua nyingine ziko kama sukari akanipa ninywe nikakataa akaninywesha na maji kwa nguvu,” anasimulia mtoto huyo.
Mtoto huyo ameongeza kuwa, mwalimu huyo baada ya kumpaka dawa sehemu hizo alivua nguo zote kama vile anaenda kuoga,ndipo alitoa dawa nyingine na kuanza kumsugua sehemu za siri ,baada ya hapo alipoteza fahamu hakujua kilichoendelea alizinduka muda wa jioni na kumuona mwalimu huyo akichungulia dirishani mara mbili kuona kama kuna watu.
Aidha mwalimu Jonas alimwambia kuwa, akipata shida yoyote amtume mdogo wake wa miaka (11) ambaye anasoma shuleni hapo ili amfikishie taarifa mwalimu aone atafanyaje na alimsisitiza asiwaambie wazazi na mtoto huyo aliondoka akaenda nyumbani na kuwaeleza wazazi wake kilichotokea.
“Nilipomchunguza mtoto wangu nilibaini ameingiliwa kimwili kwanza alikuwa natembea kwa kuchechemea akisema anapata maumivu sehemu za siri pia niligundua michubuko sehemu zake za siri,” amesema mama wa mtoto huyo nakuongeza:
“Baba wa mtoto alipofika nyumbani nilimueleza yaliyomsibu binti yake,tukaamua kwenda kituo cha polisi Muleba,tukapewa fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya kwenda hospitali kufanyiwa vipimo,ndipo tulipompeleka kituo cha Afya Kaigara,”.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa