Na Ashura Jumapili,TimesMajira online Kagera ,
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Kagera(WJK),kimemuibua mtoto wa miaka 13 muhitimu wa darasa la Saba,wilayani Muleba mkoani Kagera,aliyefanyiwa ukatili na mwalimu wake baada ya kunyweshwa kitu kinachodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya kisha kupoteza fahamu na kubakwa akiwa darasani.Ambapo baada ya mtuhumiwa huyo kutekeleza kitendo hicho alitoweka kusikojulikana.
Inadaiwa mtoto huyo alifanyiwa ukatili huo,Oktoba 30, mwaka huu majira ya jioni, baada ya mtoto huyo akiwa na wanafunzi wenzake kufika shuleni hapo majira ya mchana kwa ajili ya kuomba mwalimu huyo wa taaluma wa shule ya msingi Rulanda,aliyejulikana kwa jina la Lameck Jonas awaangalizie matokeo ya mtihani wa darasa la saba.Kwani Binti huyo na wenzake walikuwa wahitimu wa darasa la Saba katika shule hiyo.
Baada ya kupata taarifa hiyo WJK, ilifunga safari na kutembea umbali zaidi ya kilomita 100 kutoka Bukoba Mjini hadi Wilayani Muleba Kata ya Rulanda,na kuzungumza na mtoto huyo,wazazi,wananchi na viongozi mbalimbali.
Mtoto huyo anasimulia”Nilirudi nyumbani nikawambia wazazi kuwa mwalimu,ameniambia nimeshindwa mtihani hivyo nirudi shuleni saa 10:00 jioni anishauri.Muda huo ulipokaribia wazazi waliniruhusu nilirudi shuleni nimsikilize mwalimu Jonas, niliporudi nilimkuta ofisini akaniambia niende kwenye darasa tulikokuwa tunasomea atanikuta,”ameeleza mtoto huyo na kuongeza kuwa:
“Nilimsubilia darasani,baada ya muda alifika nakuanza kufunga madirisha na mlango,kisha akaniambia nivue nguo,nikakataa akanifungua zipu akaanza kunipaka dawa kwenye shingo, matiti, kwapani na kwenye kitovu, akatoa nyingine akanipaka mgongoni, alipomaliza akachukua nyingine ipo kama sukari akanipa ninywe,nikakataa akaninywesha na maji kwa nguvu,”.
Ameeleza kuwa mwalimu huyo baada ya kumpaka dawa sehemu hizo,alivua nguo zote kama vile anaenda kuoga,kisha alitoa dawa nyingine na kuanza kumsugua sehemu za siri. Baada ya hapo mtoto huyo anasimulia kuwa alipoteza fahamu na hakujua kilichoendelea, alizinduka muda wa jioni na kumuona mwalimu huyo akichungulia dirishani mara mbili kuona kama kuna watu.
“Alipooona hakuna watu,aliniambia niende nyumbani,nikipotoka nje aliniita ana.kuniambia baba na mama yangu wakiniuliza,sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani ,niwadanganye kuwa nilienda kwa rafiki zangu.Pia wakiniuliza kuhusu mdomo kukauka niseme ndivyo ulivyokuwa na hata wakiniuliza kuhusu kuchechemea kutokana na maumivu ni jibu ndivyo ni avyotemvea au nimeanguka,”.
Hata hivyo mtoto huyo anadai kuwa, mtuhumiwa huyo(Mwalimu), alimwambia kuwa akipata shida yoyote,amtume mdogo wake mwenye umri wa miaka 11, ambaye anasoma shuleni hapo ili amfikishie taarifa aone atafanyaje,na alimsisitiza asiwaambie wazazi. Lakini binti huyo aliwaeleza wazazi wake baada tu ya kufika nyumbani.
Kwa upande wake mama wa mtoto huyo mkazi wa kitongoji cha Kituntu kata ya Rulanda,amesema kuwa, ilipofika saa 11:30 jioni aliona mtoto anachelewa kurudi nyumbani,ndipo aliamua kumfuata shuleni bila mafanikio
“Nilipofika shuleni niliona pikipiki ikiwa imepakiwa nje,sikusikia kelele kwenye mazingira yale na sikuona mtu yeyote,nilidhani ile pikipiki ilikuwa ya mtu ambaye alikuwa ameenda ziwani,hivyo niliamua kurudi nyumbani nikawa na maswali mtoto ameenda wapi mbona siyo kawaida yake kufika mpaka muda huu hayupo nyumbani,”.
Ameeleza kuwa,ilipofika saa 1:00 jioni,mtoto alifika nyumbani ambapo alimuhoji,na kumjibu kuwa alikuwa shuleni kwani mwalimu Jonas alimfungia kwenye chumba cha darasa na kumpaka dawa sehemu mbalimbali za mwili wake na kuwa alimbana midomo asipige kelele.
“Nilipomchunguza mtoto wangu,nilibaini ameingiliwa kimwili na michubuko sehemu za siri,pia alikuwa anatembea kwa kuchechemea huku akidai kupata maumivu sehemu za siri.Baba yake alipofika nyumbani,nilimsimulia yaliyomsibu binti yake,tukaamua kwenda kituo cha polisi Muleba,tulipewa fomu namba tatu ya polisi (PF3),kisha tukampeleka kituo cha Afya Kaigara kwa ajili ya vipimo,”.
Hata hivyo mama huyo anadai kuwa ,baadhi ya ndugu wa mtuhumiwa waliojitambulisha kama kaka na rafiki zake,walifika nyumbani kwao kwa ajili ya kuomba walimalize jambo hilo kwa ahadi ya kuwapa kiasi cha fedha ambacho hawakutamka ni kiasi gani
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Muleba ambaye ni mwajiri wa mtuhumiwa huyo,Isaya Mbenje amesema, alipokea taarifa kutoka shule ya msingi Rulanda kwamba kuna tuhuma za mwalimu Lameck Jonas kufanya tendo la ukatil.
Mbenje,anasema, taarifa za awali zinaonesha mwanafunzi huyo amemaliza darasa la Oktoba mwaka huu shuleni hapo,bahati nzuri wazazi wake walipata taarifa kwa wakati na kutoa taarifa kituo cha polisi,huku mtuhumiwa huyo anaendelea kutafutwa.Na yeye kama mwajiri wake anamtafuta kwa ajili ya kuhakikisha anafikishwa kwenye vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake.
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Rulanda Evart Ernest,alisema kuwa, alipokea taarifa za mtoto kubakwa Oktoba 31, mwaka huu majira ya saa 12:30 asubuhi kutoka kwa Ofisa Elimu Kata,aliyempigia simu juu ya tukio hilo na kumjulisha kuwa tayari hati ya kumkamata mtuhumiwa kutoka jeshi la polisi imetolewa.
“Nilipomtafuta mzazi alisema ameenda kwa mytendaji wa Kijiji kwa ajili ya kumkamata mtuhumiwa saa 11:00 alfajiri,hakufunguliwa mlango hadi alipompigia yeye saa 2:00 asubuhi na kumuhoji kulikoni ndipo Mtendaji alimjibu alikuwa anaoga.Ukiangalia muda huo unaona kama kuna tatizo, haiwezekani mtu umwamshe tangu saa 11:00 alfajiri hadi saa 2:00 asubuhi adai alikuwa anaoga, uzembe huo ndiyo ulisababisha mtuhumiwa kutoroka kabla hajakamatwa,”ameema Ernest.
Alipohojiwa kama kuna matukio mengine ya ubakaji katika kata yake,Diwani huyo amesema kuwa, hilo ni tukio la kwanza labda matukio mengine ya ukatili yapo kama vile wazazi kutelekeza familia, vipigo vilivyopitiliza na watoto kutumikishwa chini ya umri.
Wilmina Projestus mkazi wa kijiji cha Rulanda amesema, vitendo hivyo vya ukatili,vimekuwa kama mazoea na wao wazazi wameanza kuogopa.Hivyo ameiomba Serikali iwe na mpango maalumu wa kudhibiti vitendo hivyo katika jamii,kwa kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu masuala ya ukatili.
Yusto Bakuju mkazi wa kitongoji Kituntu amesema, kitendo cha ukatili alichofanyiwa mtoto huyo ni unyama unaolenga kumkatisha tamaa katika maisha yake sababu bado ni mdogo na ana ndoto nyingi na unaweza kumuathiri kisaikolojia.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda, alipotafutwa kwa njia ya simu amesema, yupo safarini kuelekea wilayani Misenyi hivyo atafuatilia na kutoa taarifa Novemba saba, mwaka huu.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote