March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwakinyo kupanda ulingoni Jijini Mwanza Disemba 26


‎Na Penina Malundo,Timesmajira


‎Bondia Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni kwenye pambano la kimataifa la Ubingwa Wa Afrika jijini Mwanza Disemba 26.2025.

‎Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam,Mwakinyo amesema anawaomba wadhamini kudhamini pambano Hilo la “BOX ON BOXING DAY” ili kukata KIU YA Mashabiki Wa ndani Na Nje ya Tanzania.

‎Kwa upande wake Mratibu wa Matukio kutoka waandaji wa pambano hilo chini ya Meja Semunyu Peak Time Bakari Khatibu amesema,Peak Time imekuwa ikikuza Vipaji vya ngumi kwa hapa Tanzania na kabla ya Pambano kuu kutakuwa na Mapambano madogo madogo katika mikoa ya Mwanza,Kahama na Kagera ili kutafuta Mabondia watakao msindikiza Hassan Mwakinyo kwenye “BOX ON BOXING DAY” Disemba 26.

‎Pambaono la “Boxing on Boxing Day” linatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza jijini Mwanza 26.Diaemba,Ambapo Hassan Mwakinyo atapanda ulingoni kwaajili ya kukata kiu ya mashabiki wa masunbwi Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.