Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Bondia namba moja nchini Tanzania, Hassan Mwakinyo ameporomoka kwa nafasi moja katika viwango vya ndondi Afrika. Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa Boxrec.
Mwakinyo ambaye tangu mwaka 2018 alikuwa kinara kwenye uzani wake kabla ya hivi karibuni kuporomoka hadi nafasi ya pili, ameporomoka tena hadi nafasi ya tatu kwenye uzani wa Super Welter.
Mabondia kutoka nchini Afrika Kusini, Roarke Knapp na Brandon Thysse ndiyo wamemporomosha Mwakinyo kileleni kwenye ubora wa uzani wa super welter Afrika.
Knapp sasa ndiye namba moja na Thysse akikamata nafasi ya pili wote wakiwa na nyota tatu na nusu sawa na Mwakinyo aliyetajwa kwenye nafasi ya tatu wakitofautiana pointi.
Aidha, Kidunia, Mwakinyo amesalia kuwa wa 43 kati ya mabondia 1960 wakati nchini akizidi kuwa kinara kwenye kila uzani ‘pound for pound’.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania