December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwakalebela apelekwa kamati ya Sheria

BAADA ya klabu ya Simba kuwasilisha malalamiko yake kufuatia kauli ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kuwa wamefanya mazungumzo na mchezaji Clatous Chama, tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepeleka malalamiko hayo kwenye Kamati yake ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambacho ndicho chombo chenye mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Katika malalamiko hayo, Simba wameomba ichukuliwe hatua stahiki ili kulinda kanuni zinazotawala mpira wa miguu pamoja na weledi kwani kanuni hizo zimeweka wazi kuwa kufanya mazungumzo na mchezaji aliye ndani ya mkataba ni ukiukaji wa Kanuni za usajili.