December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwakajoka:Fedha zilizokuwa zinakatwa na viongozi CHADEMA zimetumika vizuri

Na Joyce Kasiki,TimesMajira Online, Dodoma

MBUNGE wa Tunduma Frank Mwakajoka amesema fedha zinazofanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) zilikuwa zinakatwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kutoka mahojiano na taasisi hiyo,Mwakajoka amesema,fedha hizo zimetumika na zinaendelea kutumika vizuri kama ilivyokusudiwa.

“Fedha hizi zilikuwa zinakatwa kwa mujibu wa katiba ya chama chetu na ninakishukuru chama changu kwamba fedha zimefanya kazi nzuri ya kukijenga chama na sasa kimepanuka kuanzia chini mpaka juu.

” Pia fedha hizi zimefanya kazi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na sasa zinaendelea kufanya kazi ya maandalizi katika uchaguzi mkuu” amesema Mwakajoka.

Wabunge ambao mpaka sasa wameshahojiwa ni pamoja na Frank Makajoka,Mbungebwa viti Maalum Suzan Lyimo huku ambao wameshafika kwa ajili ya mahojiano ni pamoja na mbunge wa viti Maalum Ruth Mollel,Mbunge wa Mlimba Suzan Kwanga,Mbunge wa Mbozi Pascal Haonga, na Mbunge wa Mikumi Joseph Mbilinyi.