November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mvua zasababisha mlima kupasuka

Na.Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Sumbawanga

MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa zimesababisha kupasuka kwa kipande cha mlima wa lyambalyamfiopa katika Bonde la ziwa Rukwa Wilaya ya sumbawanga na kusababisha watu wawili wa familia moja kufariki dunia katika kitongoji cha Kamoko Kata ya Muze baada ya kufukiwa na tope zito lilitokana na maporoko ya maji huku nyumba 38 zikianguka katika kata ya kapenta.

Wakazi wa kijiji hicho katika nyakati tofauti wamesema licha ya hilo mvua hiyo imeharibu mazao na baadhi ya nyumba kuharibiwa na watu 15 kujeruhiwa.

Mganga Mfawidhi wa zahanati ya kijiji cha Uzia Dkt.Maiko Mwaipora amesema amewapokea watu 15 ambao wamejeruhiwa na watu wawili wakiwa wamefariki dunia na kuelezea hali za wagonjwa.

Hata hivyo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo imetembelea maeneo hayo, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile,amewataja waliofariki duinia kuwa ni Sai Weja ( 26) na Geshi Gwesu mwenye umri wa miaka 7 wote wakazi wa kijiji cha Uzia.

Aidha amesema licha ya hilo nyumba 38 zimeanguka katika Kata ya Kapenta kutoka na mvua hizo.