January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zao la tumbaku

Mvua yasababisha tumbaku kupungua uzito Chunya

Na Esther Macha,Timesmajira,Online ,Chunya

CHAMA Kikuu cha Wakulima wa Tumbaku (CHUTCU) wilayani Chunya mkoani Mbeya kimesema msimu wa kilimo uliopita hali ya uzalishaji ilikuwa mbaya kutokana na mvua nyingi kunyesha, hivyo kusababisha zao hilo kupungua uzito.

Kaimu Meneja wa chama hicho, Juma Nshinshi amesema msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19 mahitaji yalikuwa kuzalisha tani milioni 9.92, lakini uzalishaji ulipunguas na kufikia tani milioni 6.

“Kimsingi msimu uliopita wakulima wetu walipata hasara kubwa sana kwa kuwa walitumia gharama kubwa za pembejeo za kilimo kama mbolea zilizombwa mna maji kutokana na mvua nyingi kunyesha,”amesema Nshinshi

Aidha, amesema bei ya tumbaku ilipungua kwa kilo kutoka dola 1.6 za marekani hadi dola 1.33 za Marekani.

Kaimu Meneja huyo amesema hali hiyo ilitokana na changamoto za kupungua ubora wa uzito wa hasa kushuka kwa soko la zao hilo.

Hata hivyo, Nshinshi amesema kufuatia changamoto hiyo msimu huu wa kilimo wamefanya maandalizi ya kimkakati ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa pembejeo za kilimo ambazo zitawafikia wakulima 7,500 walio katika vyama vya ushirika 23 waliopo wilayani hapa.

Amesema lengo ni kuona msimu huu wakulima wanafutwa machozi kwa kuzalisha kwa wingi na kuwepo kwa soko la ndani na nje ya nchi.

“Tayari kuna kampuni tumeingia nazo mikataba ya kununua tumbaku kupitia chama chetu na mawaka ambao wameanza kupokea pembejeo za kilimo, hivyo tuna sababu ya kuwasimamia wakulima kuzalisha kwa kiwango cha hali ya juu ili kuuza kwa bei nzuri na elekezi ya Serikali,”amesema

Mkulima wa tumbaku, Salome Kilasi amesema msimu huu wa kilimo Serikalui iongoze nguvu kwa kuhakikisha wakulima wanafikiwa na pembejeo za kilimo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwabnana mawakala wanaouza pembejeo feki.