Mkazi wa Mjini Tanga anayefanya biashara ndogondogo ya kuuza matunda, Salim Ndaro ‘kama zali’ vile amejishindia zawadi shilingi milioni 10, katika Kampeni ya Magifti Dabodabo inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo.
Akielezea furaha yake kwa ushindi huo alipokuwa akikabidhiwa mfano wa hundi ya pesa alizojishindia sambamba na kuingiziwa kiasi hicho kwenye Tigo Pesa yake mfanyabiashara huyo aliyekuwa akiishi kwenye nyumba yake ya nyasi amesema pesa hizo zitamfanya abadili maisha na kumfanya aachane na kuishi kizamani na kuikarabati nyumba yake hiyo iwe na muonekano wa kisasa.
Mshindi huyo ameendelea kusema kuwa ushindi huo uwe chachu kwa wateja wengine kuendelea kushiriki kampeni hiyo ya Magifti Dabodabo kwa kutumia huduma mbalimbali za Tigo kama vile huduma za Tigo Pesa, Kufanya manunuzi kwa Lipa namba, kulipa bili, kuongeza salio na nyinginezo ambapo kumbe mtu yeyote anaweza kujishindia kama alivyojishindia yeye.
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Tigo Kanda ya Pwani, Abdul Ally baada ya kumpongeza mshindi huyo amesema zawadi hizo zitaendelea kutolewa kwa washindi kampeni hiyo na kuzitaja zawadi hizo kuwa ni pesa taslimu shilingi milioni moja, milioni 5, milioni 10, seti ya vifaa vya nyumbani kutoka kampuni ya Hisense ikiwemo friji, microwave, tv na redio ya muziki wa kisasa (Sound Bar) na magari mapya kabisa na ya kisasa.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu