Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Tanga
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapindizi(CCM),Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewahakikishia wananchi wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga, kuendelea kupata miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu na miundombinu ya barabara.
Dkt. Nchimbi amesema hayo Septemba 16, 2025,kwenye mkutano na wananchi wa Jimbo hilo, uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee uliopo wilayani ya Muheza mkoani Tanga, akiendelea kukinadi chama hicho,ambapo amesema katika afya upo mpango wa uboreshwaji wa hospitali ya wilaya na kuiongezea hadhi.

Pia ujenzi wa vituo vitatu vya afya na zahanati 10, ambapo kwa upande wa elimu amesema upo mpango wa kuongeza shule za msingi 10 na sekondari tano, madarasa 215 katika shule za msingi na madarasa 115 katika shule za sekondari.
Pia ameendelea kuelezea kuwa, katika Wilaya hiyo miradi 12 ya maji itaanzishshwa ambapo visima virefu vitachimbwa, ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji.
Dkt. Nchimbi amesema, skimu za umwagiliaji zinaenda kuongezwa ikiwa pamoja na ruzuku ya mbolea, mbegu na madawa, ambapo katika upande wa ufugaji, chanjo na tiba ya mifugo inaenda kuboreshwa kwa kuongeza sehemu za kuogeshea mifugo ‘majosho’ na mabwawa pamoja na kutenga maeneo maalumu ya malisho na mifugo.

kwa upande wake mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza kupitia CCM Hamis Mwinjuma Maarufu (Mwana FA), amesema, wananchi wa Muheza wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko la mazao, hali inayosababisha mazao kuharibika kwa haraka hususani machungwa na viungo.
Ambapo Dkt. Nchimbi amewaahidi changamoto hiyo kutatuliwa mapema endapo wananchi wataichagua CCM kwa mara nyingine tena.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako