Na Heri Shaaban,Timesmajira. Online
MUFTI wa Tanzania Shekhe, Abubakary Zuberi amewataka Watanzania kudumisha amani na mshikamano na pia wasichafue hali ya hewa nchini.
Mufti ameyasema hayo Dar es Salaam katika Kongamano la Dini ya KiislamU lililoandaliwa na Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Kituo cha Kiislamu cha Misri.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mufti amesema tunajivunia amani iliyopo nchini hivyo tudumishe amani iliyopo na umoja uliopo na isitokee baadhi ya watu kuchafua hali ya hewa.
“Amani ndiyo jambo la msingi sana, nawaomba Watanzania tudumishe umoja na mshikamano wetu na tuzidi kuchapa kazi katika kuisaidia serikali yetu na kuunga mkono Juhudi za Rais, Samia Suluhu Hassan,” amesema.
Amesema amani iliyopo nchini ni lulu hivyo Watanzani wanatakiwa kuendelea kudumisha mshikamano na kujenga uzalendo kwa ajili ya nchi.
Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema Uislam kuchafuliwa si vizuri na kila moja anahitaji amani, wanyama na ndege pia wanahitaji amani kwa na ndiyo maana mtu anapomfuata ndege wa aina yoyote au kunguru anaruka.
Shekhe Salum amesema, Waislamu na Afrika wanaendelea kuombea amani Tanzania na Afrika kwa ujumla huku wakijenga mahusiano mazuri.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu cha Misri Tanzania, Shekhe Jamal Abdulmdaty amesema mafunzo hayo ya dini yanawafunza Waislamu kwamba ni dini ya kweli hivyo wanatakiwa kusaidiana katika wema na wale ambao si Waislamu pia wasaidiane mtu atakayemuua mwezanke hawezi kuona pepo.
More Stories
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa