April 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Muft Zuberi amewataka BAKWATA Vingunguti kulinda amani

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

MUFTI Mkuu wa Tanzania Dkt.Abubakar Bin Zuberi, amewataka viongozi wa BAKWATA Vingunguti na watanzania kulinda amani ya nchi.

Huku akitoa wito wa kujengwa kwa ofisi ya BAKWATA ngazi ya kata nchini nzima,kwani ndipo walipo wananchi.

Dkt.Zuberi,amesema hayo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya BAKWATA Kata ya Vingunguti wilayani Ilala jijini Dar-es+Salaam.

“Nawataka viongozi kujishusha kwa wananchi, nawaomba BAKWATA Vingunguti kulinda amani ya nchi pamoja na Watanzania kwa ujumla,tuzingatie misingi ya dini yetu katika suala la amani ya nchi yetu,”amesema Zuberi.

Amesema shughuli za watu zinaanzia chini hivyo amewataka waumini wa dini hiyo ya kuwa na katiba ya BAKWATA pamoja na kutumia vizuri ofisi hiyo ya Vingunguti.

Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar-es-Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti wilayani Ilala, amesema hivyo kalribuni Vingunguti itakuwa ya kisasa na kupata maendeleo ikiwemo barabara za kiwango cha lami pamoja na kufungwa taa barabarani.

Amesema katika kipindi cha miaka, serikali imepeleka kiasi cha milioni 900 Kata ya Vingunguti kwa ajili ya miundombinu ya sekta ya elimu,ambapo zimejengwa shule mpya za sekondari na msingi.

Pia mradi wa Machinjio Vingunguti, imepeleka bilioni 2 ambapo pia amesema hivi karibuni mbolea itauzwa katika machinjio hayo na soko la Mbuzi la kisasa litajengwa.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo amesema,uwepo wa ofisi hiyo ya BAKWATA itachochea amani Vingunguti na Ilala kwa ujumla.