December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtoko wa kibingwa wa Betika waendelea kushika kasi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mtoko wa Kibingwa msimu wa tano wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betika unaendelea na katika msimu huu Kampuni hiyo inahitaji idadi ya Mabingwa 100 ili kushuhudia mtanange wa Simba dhidi ya Yanga katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Aprili 16, 2023.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa Umma wa Kampuni hiyo, Juvenalius Rugambwa amesema katika wiki ya kwanza ya Promosheni hiyo kulikuwa na droo tatu huku droo hizo wakipatikana jumla ya washindi watano, washindi hao ni Mariamu kutokea Chamazi, Dar es Salaam, Fahame (Simiyu), Clement (Songea), Steven (Kagera) na Joshua Charles (Mkuranga, Pwani) hivyo wamebaki washindi 95 ambao wanahitajika.

Rugambwa amesema washindi hao ambao watatokea mikoani watapatiwa Tiketi za Ndege kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo wa Dabi ya Kariakoo na watalala kwenye Hoteli ya Nyota tano wakiwa jijini Dar es Salaam.

“Kushiriki kwenye droo, mshiriki anatakiwa kubashiri mikeka mitano kila siku na kwa kila mkeka unatakiwa kuweka kiasi cha Shilingi 500/- na zaidi hivyo utaendelea na utapata nafasi ya kuingia kwenye Mtoko wa Kibingwa,” amesema Rugambwa

Amesema unaweza kubashiri katika Ligi zote duniani kama vile Ligi ya Uingereza (EPL), Ligi ya Hispania (La Liga), Ligi ya Ujerumani (Bundesliga), Ligi ya Ufaransa (Ligue 1), Ligi ya Italia (Serie A) sanjari na michezo ya ‘NBC Premier League’. Hata hivyo, amesema droo nyingine zitafanyika Februari 20, 22, na 24 mwaka huu na kupatikana washindi 10 katika wiki.

Ili kubashiri michezo mbalimbali unapaswa kutembelea Tovuti ya www.betika.co.tz ili kupata fursa ya kubashiri au unaweza kupiga 14916# Mtoko wa kibingwa msimu wa tano.

Afisa Mahusiano na Umma wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa Akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuchezesha droo ya tatu ya Kampeni ya Mtoko wa Kibingwa iliyochezezhwa katika studio za East Africa Radio Mikocheni Jijini Dar es salaam