May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtemvu awataka Wanawake kusimamia ndoa zao

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM mkoa Dar es Salaam ,Abbas Mtemvu ,amewataka Wanawake kusimamia ndoa zao Ili wawe na heshima kwa Wanaume zao .

Mwenyekiti Abbas Mtemvu alisema hayo katika semina ya ujasiriamali iliyoandaliwà na Diwani wa Viti Maalum wanawake Wilaya ya Ilala Julieth Banigwa kwa ajili ya Umoja wanawake UWT iliyofanyika Jimbo la Segerea ambayo umewashirikisha Makatibu wa UWT ,Wenyeviti wa UWT ngazi ya kata kutoka Wilaya ya Ilala

“Ninawashauri Wanawake msijisahau katika kusimamia ndoa zenu Ili muwe na heshima kwa wanaume zenu muweze kutunza ndoa zenu msidanganyike “alisema Mtemvu .

Akizungumzia Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala aliwataka UWT kuongeza wanachama kwani Wanawake ni Jeshi kubwa katika chaguzi mbali mbali za chama .

Alisema mwaka 2024,CCM itashinda Viti vyote Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa kushika dola 2025 CCM itashinda majimbo yote kumi hivyo aliwataka Wana CCM wawe karibu na Wananchi na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM .Aliwataka UWT na CCM kuwapa ushirikiano viongozi wao pamoja na kujenga mahusiano mema ndani na nje .

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Julieth Banigwa alisema dhumuni la mafunzo hayo walikuwa wakifundishwa ujasiriamali pamoja na elimu ya unyanyasaji kijinsia watumie Elimu hiyo kwa ajili ya Jamii .

Diwani Julieth Banigwa alisema mafunzo hayo sawa na kuwapa nyavu ya samaki sasa kazi kwao kwenda kuvua waepeleke chini kuwapatia Jamii .”Mimi Diwani wa Viti Maalum Julieth Banigwa tunafuata nyayo za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .

Samia Suluhu Hasaan katika kuwakomboa Wanawake wa Wilaya ya Ilala kufanya siasa na kuwakwamua kiuchumi “alisema Banigwa .Mwenyekiti wa Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa alimpongeza Diwani Julieth Banigwa kwa kuwawezesha Wanawake katika mafunzo hayo ya kiuchumi .

Mwenyekiti Neema Kiusa aliwataka wanawake waache kuwa tegemezi badala yake wajikwamue kiuchumi katika kuzalisha shughuli za ujasiriamali pia washirikiane na kujenga umoja na mshikamano.