January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtanzania azidi kuomba msaada wa Rais Dkt. Samia

Na Mwandishi Wetu, TimesMajiraOnline,Dar

MTANZANIA aishiye Ujerumani, Lucy Koble aliyeomba msaada kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezidi kuomba msaada kwa kiongozi huyo mkuu wa nchi kwani tangu alipotoa kilio chake mwaka jana, hajapata msaada wowote kwake wala kwa mtoto wake.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka katika jiji la Munic nchini Ujerumani, Lucy amdsema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na ubalozi haujampatia msaada ili kuweza kutatua matatizo yake.

“Mimi pamoja na mtoto wangu tunaendela kuteseka, tangu mwaka 2016 tumekuwa tukiwakilisha maombi yetu kwa ubalozi wetu huku Ujerumani, lakini hatujasaidiwa,” amesema .

Ameongezea kuwa yeye na mwanae yamekuwa hatarini kabla na baada ya kujikuta akiwa chini ya utumwa utumiao wireless micro-sensors/implants, bila hiari na makubaliano yake kama ilivyo sheria huko aliko na sheria zote zihusikanazo na haki za binadamu duniani.

“Nimeshawasiliana na Waziri wetu wa Mambo ya Nje lakini naye amesema niwasiliane tu na Ubalozi wetu uliopo huku huku Ujerumani wao ndiyo watanisaidia, lakini sijasaidiwa ,” amesema.

Amesema hivi karibuni, Lucy alimwandikia Barua Rais akisema kuwa yeye pamoja na mtoto wake, wanahitaji msaada baada ya kuwekewa mwilini mwao bila ruhusa zao vifaa vinavyojulikana kama “wireless body Area micro- sensors/implants” ama “Theranostic sensor/implants”, ambavyo katika utaratibu wa afya hutumika kufanyia uchunguzi ili kutathmini tiba maalum za magonjwa na au kuendeleza tiba na uanglaizi wa wagonjwa wenye magonjwa ya
kudumu.

“Ila, sisi si wagonjwa. Ubadhilifu huu tulitendewa na
watu ambao mpaka sasa hawajajulikana. Tumekuwa tukitumika kama wanyama wa maabara, tukiumizwa na kuteswa na hao wavunjao sheria ya haki zetu sisi kama binadamu,” alimweleza Rais
katika Barua yake.

Ameongezea kuwa majaribio yanayofanyika yanahusisha maumivu makali sana mwilini na hali mbaya sana kiafya. Haki zao za uhuru wa
kibinadamu zimepotea.

“Na si hizi tu zitakazoendelea kupotea bali pia, maisha yetu yako hatarini kupotea, kama serikali yetu haitatoa msaada au kuingilia kati.

Ninakimbilia wewe Rais, kwa sababu juhudi zangu mwenyewe katika kutafuta msaada kwa muda mrefu sana hazijaleta matokeo yanayoweza kutusaidia.” Amesema Lucy.

Baadhi ya vifaa hivi ni vya matoleo ya kisasa kabisa katika teknolojia ya jinsi hii ya kipekee, ambayo imefanya mkondo wa kisayansi unaouhusiana na sera na mifumo ya afya katika baadhi ya nchi zipate hatua mpya za kimaendeleo, hasa kwa sababau ya kuokoa muda wa mawasiliano baina ya madaktari na wagonjwa, na kuweza kukata matumizi makubwa ya kifedha.

Wao wamekuwa wakitumika kama wanyama wa majaribio ya kuendeleza matangazo, mauzo na kuboresha ubunifu katika sekta hii na nyinginezo zinazohusika.