December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtanzania aishie Ujerumani amuomba Rais Samia msaada

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Onlime, Dar

MTANZANIA aishie nchini Ujerumani, Lucy Sharon Köble amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan msaada wa dharura kutokana na yeye na mwanaye maisha yao kuwa hatarini baada ya kujikuta wakiwa chini ya utumwa utumiao wireless micro-sensors/implants, bila hiari na makubaliano yake kama ilivyo sheria huko aliko na sheria zote zihusikanazo na haki za binadamu duniani.

Katika barua yake kwa Rais, Mtanzania huyo alisema; “Mheshimiwa Rais Samia nakuomba uchukue fursa uangalie bango langu. Mimi pamoja na mtoto wangu, tunahitaji msaada baada ya kuwekewa miilini mwetu bila ruhusa zetu vifaa vinavyojulikana kama “wireless body Area micro-sensors/implants” or
“Theranostic sensor/implants”, ambavyo katika utaratibu wa afya hutumika kufanyia uchunguzi ili kutathmini tiba maalum za magonjwa na au kuendeleza tiba na uangalizi wa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu.

Lakini sisi si wagonjwa. Ubadhilifu huu tulitendewa na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana,” ameeleza Lucy kwenye taarifabarua hiyo na kuongeza;

Tumekuwa tukitumika kama wanyama wa maabara, tukiumizwa na kuteswa na hao wavunjao sheria ya haki zetu sisi kama binadamu. Kwa sasa wanaweza kwa njia rahisi kabisa, bila kujulikana kufanya maovu yao, kwa mfano: cyber-slavery, e-human-trafficking, e-stalking, e-abduction, e-torture, e-terrorism, e-tracking and monitoring, e-slavery nk., kwa kupitia computer na mitandao ya satelaiti.

Majaribio yanayofanyika yanahusisha maumivu makali sana mwilini na hali mbaya sana kiafya. Haki zetu za uhuru wa kibinadamu zimepotea. Na si hizi tu zitakazoendelea kupotea bali pia, maisha yetu yako hatarini kupotea, kama Serikali yetu haitatoa msaada au kuingilia kati.”

Amesema amemkimbilia Rais Samia kwa sababu juhudi zake mwenyewe kutafuta msaada kwa muda mrefu sana hazijazaa matokeo yanayoweza kuwasaidia.

Kwa mujibu wa Mtanzania huyo, suala hilo linajulikana kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambako pia aliwasilisha kwa kadri ya fursa alizopata.

Amesema ni miaka karibu sita imepita tangu alipoanza kuomba msaada kutoka ubalozini nchini Ujerumani na kutoka kwa wizara Mambo ya Nje. “Ninazo taarifa za kuaminika kuwa sisi nasi (Tanzania), tunao uwezo wa kushughulikia teknolojia kama hizi.

Pamoja na taarifa kuwa serikali yetu iko wazi kutusaidia, maombi yangu yamepata vikwazo kwa sababu mbalimbali,”amesema na kuongeza;

“Naiomba Serikali yako tukufu iliangalie hususan juu ya kutimizwa kwa uchunguzi ili tujue lile lililoleta hitimisho kama hilo. Taarifa hizi zinajulikana kiuwazi na Ubalozi wetu.

Lucy amesema kwamba, yeye na mwanae wanapitia mateso makubwa kwa karibu muda wa miaka 21 sasa na kujua chanzo cha matatizo hayo kumechukua muda mrefu sana kwa kuwa ridhaa yake haijawahi kuombwa.

Amesema baadhi ya vifaa hivyo ni vya matoleo ya kisasa kabisa katika teknolojia ya aina hiyo ya kipekee, ambayo imefanya mkondo wa kisayansi unaouhusiana na sera na mifumo ya afya katika baadhi ya nchi zipate hatua mpya za kimaendeleo, hasa kwa sbabau ya kuokoa muda wa mawasiliano baina ya madaktari na wagonjwa, na kuweza kukata matumizi makubwa ya kifedha.

Alisema yeye na mtoto wake wameteuliwa kwa ajili ya tafiti mbalimbali na vipimo vya kliniki zinazohusisha DNA/Genes, matumizi mabaya ya viungo mbalimabli vya mwilini (ubongo, moyo, n.k).

Tafiti nyingine zinahusu mifumo ya neva na mishipa ya damu, maandalizi ya upasuaji wa wengine au binafsi, upotoshaji wa kiitikadi za kisiasa, tabia binafsi, uchambuzi wa fikra ili kupata mateka au watumwa, wa misimamo inayowapendeza hawa watu, n.k.

Vifaa hivi viko hai; vinawasilisha na kuwasiliana na mifumo ile ya majambazi. Hatuna ulinzi wowote. Miili yetu iko wazi kwa watu tusiowajua kwenye computer zao. Uhuru wetu unamilikiwa. Mimi ni mtu mzima; mwanangu wanae tangu kama siku moja au mbili baada ya kuzaliwa.

“Imenichukua muda mrefu kuchukua hatua za kutafuta msaada kwa kuwa sikujua ni kipi kilikuwa kikiendelea. Pia, hata nilipojua, ilinichukua muda kutafuta msaada toka nchini kwetu.

Alisema wakati anaadika mateso ya namna kadhaa yanaendelea, yameongezeka. wakati mwili wake na mwanae unatumiwa kuinufaisha miili ya watu wasiowajua.

“Kwa sababu ya hili na mengineyo niliyokwisha ya elezea, nakuomba, Mheshimiwa Rais, uingilie kati kwa mamlaka uliyonayo. Naamini wewe ni mwenye huruma na una upeo wa utambuzi, una hekima, busara na weledi mkubwa unaohitajika.

Kama raia chini ya uongozi wako, naichukua hatua hii pia kuweka wazi suala hili kama sehemu yangu ya uwajibikaji na uungaji mkono uongozi wako ili isije ikawa masuala kama haya hayakufikii kwa sababu moja au nyingine.

Alisema kama mzalendo, anaona haja ya kuomba Serikali kuweka uzito wa kusimamia migogoro ya namna hiyo.

Alisema ana imani na Rais Samia kwamba anaweza kulitatua hili jambo hilo. “Naamini kuwa kama kuna mtu anahitaji kupata ufahamu kamili haswa juu ya mambo haya pia, basi mmoja wapo ni wewe. Naamini kuwa taarifa na maombi haya yanao uwezo wa kukusaidia kulikinga taifa letu na uovu huu na madhara yake,” amesema

Nakushukuru sana kwa hatua yeyote utakayochukua kuhakikisha tumesaidiwa kutoka katika utumwa huu, hali imekuwa mbaya sana. Nakutakia kila la kheri. Mwenyezi Mungu akufanikishe katika kazi zako zote na hata katika maisha yako binafsi,” alisema Lucy.

Lucy Sharon Köble

KUHUSU VIFAA HIVYO

Amesema baadhi ya vifaa hivyo ni vya matoleo ya kisasa kabisa katika teknolojia ya aina hiyo ya kipekee, ambayo imefanya mkondo wa kisayansi unaouhusiana na sera na mifumo ya afya katika baadhi ya nchi zipate kupiga hatua mpya za kimaendeleo, hasa kwa sababau ya kuokoa muda wa mawasiliano baina ya madaktari na wagonjwa na kupunguza matumizi makubwa ya kifedha.

“Sisi tumemekuwa tukitumika kama wanyama wa majaribio ya kuendeleza matangazo, mauzo na kuboresha ubunifu katika sekta hii na nyinginezo zinazohusika,” amesema Lucy na kuongeza;

Njia mojawapo wanayotumika kupitia mifumo hii, ni kwa kuigia kwenye miili ya watu kusikokuwa na magonjwa ili kuweza kuona jinsi magonjwa fulani fulani yanavyoaanza ili kuweza kusaidia ubunifu wa tiba, n.k.”

Kama mtu anayejaribiwa hajaui chanzo cha maumivu yanayoambatana na majaribio haya, anaweza kukimbilia hospitalini na wakati mwingine hata kuwa tayari kupata operesheni zisizohitajika au hata kuondoa viungo vizima.

Mtu anaweza kujisikia kuwa mgonjwa kila wakati. “Katika ubadhilifu huu, DNA/Genes zetu zimekuwa si za siri tena, jambo ambalo linamaanisha kuwa hata DNA na GENES za Watanzania wengine, zinaweza pia kuwa hatarini.

Alisema mradi huo umeishakuwa mkubwa ambao unawaingizia majangili hao mamilioni ya fedha wakati wote waliokuwa navyo hivi vifaa.

Mimi na mtoto wangu hatujawahi kunufaika na mapato yoyote yale. Tumekuwa tukitumiwa tu, wakati wote (24/7) tangu tulipopachikwa vifaa hivyo miilini mwetu.

Pamoja na kwamba kama vifaa hivi vikitumika kama inavyopaswa mgonjwa hupewa kifaa chake mweyewe cha kumpa uhuru wa uamuzi juu ya mambo kadhaa, sisi hatujapewa faida hii na hivyo hatuna uhuru wowote wa faragha kimawazo/kifikra au kimatendo,” amefafanua na kusisitiza;

“Sisi hatuna uhuru wowote juu ya miili yetu. Sisi hatuna ulinzi wowote, na vifaa hivi vinaweza kuwasiliana na mtu yeyote, toka mahali popote duniani. Mara nyingi ninaelezwa kuwa chaneli nyingi zinatumika kwa wakati mmoja, kwa mfano katika kuweza kukifikia kiungo kimoja. Mimi ni mtu mmoja. Juu ya kinachofanywa hapo, na nani wanahusika, sijawahi kufahamishwa.

Hizi micro-sensor/implants ambazo mimi na mwanangu tumewekewa miilini mwetu huku Ujerumani ni ndogo sana, na ni maendelezo ya aina za zamani ambazo zilikuwa zikijulikana kama “help-alerts”, zilizotumika kwenye sekta za afya.

Hizi micro-sensor/implants zina mifumo ya redio ambazo zinatumika katika kuwezesha mawasilaino katoka umbali tofauti.’

Kwa kujibu wa wataalam sasa umefikia wakati ambapo ubunifu mahsusi umewezesha vifaa kama hivi pia kuweza kutumika katika maeneo mengine kama vile baadhi ya michezo (kwa wanamichezo), jeshi na ulinzi, ujenzi na ukandarasi, shughuli za migodi, usanii na tamaduni, zimamoto, magari ya wagonjwa, shughuli za usafiri wa anga, uchunguzi na utabiri wa hali ya hewa, mawasiliano na IT-Services, taasisi za fedha, lishe na famasia, usafiri wa bara na majini, (logistics, delivery chains), saikolojia, biashara na mauzo ya jumla au mengineyo, masuala ya elimu na taaluma maalum, mambo ya kilimo, ufugaji, uvuvi, n.k.

Hizi, micro-sensors ni teknolojia ambazo zinatarajiwa kuweka sura na hatua mpya juu ya jinsi mambo mengi katika huduma za kiafya (na nyinginezo) zitakavyokuwa kwa siku za mbele ili kurahisisha tiba na kupunguza muda au kukata kabisa matumizi makubwa ya fedha.

Matarajio haya ni makubwa duniani na faida nyingi zimeshanza kutathminiwa.
Wengine wanasema zitawasaidia kutengeneza magonjwa haraka ili wapate pesa haraka.

Madaktari na wauguzi wataweza kuwasiliana na wagonjwa toka karibu au mbali kama makubaliano baina yao tatapitishwa.

“Ili janga hili lilonipata mimi na mwanangu liweze kueleweka vizuri katika kusaidia kupata utatuzi na kurejesha haki zilizo dhulumiwa, ni muhimu kupata ufahamu juu ya aina halisi ya vifaa hivi.

Ni vema kupata kujua hati miliki za uvumbuzi, madai ya hati miliki na ufafanuzi wake kama zilivyotolewa rasmi. Ni vizuri pia kujua bei zake za awali na bei zake za sasa.

Ni vizuri kufahamu ni kwa nini hizi na si nyingine. Kupata fursa ya kuona jinsi sisi au binadamu wengine wanavyoonekana kwenye computer na kushuhudia jinsi miili yao ilivyounganishwa na computer, kutafunguwa macho zaidi.