November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtafiti Mutasa aiomba Serikali kufanya marekebisho sheria ya madeni

Na Mwandishi Wetu,Times Majira Online

MTAFITI Dkt. Felician Mutasa ameiomba Serikali kufanywa marekebisho kwa sheria ya madeni ili kuweka uwazi , uwajibikaji na nidhamu katika ukopaji na ulipaji madeni.

Hayo yamesemwa leo katika semina ya Vijana kutoka taasisi mbalimbali za vyuo vikuu iliyoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya kufuatilia Madeni na Maendeleo (TCDD).

Mkurugenzi Mtendaji wa TCDD Hebron Mwakagenda akifafanua jambo kuhusu deni la taifa katika seina ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali na viongozi wa dini iliyoandaliwa na taaasisi hiyo.

Dkt.Mutasa amesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya sheria ya madeni ili kulipa nguvu bunge kushiriki katika mchakato wa ukopaji wa madeni kwakuwa itasaidia fedha hizo kutumika kama ilivyokisudiwa.

“Nchi haikatazwi kukopa lakini kinachohitajika ni kukopa kwa tija na ili kuleta nidhamu katika jjambo hili ni vema Bunge likashiriki katika nchakato mzima,” amesema.Mutasa.

Mutasa amesema ili.kujenga uelewa na kusukuma uwazi wa deni hilo nchi nne za Afrika Mashariki zimefanya utafiti wa takwimu za madeni ambapo mchakato wa kuandaa vitabu utakamilima hivi karibuni.

Aliongeza kuwa, ukopaji wenye nidhamu utasaidia serikali kutoa huduma bora na kuinua uchumi wa nchi yake.

Amesema kila.nwaka bajeti ya Serikali imekuwa ikitumika kupunguza kulipa.deni hilo jambo ambalo linazidi kuchangia kuchelewa kukua kwa uchumi.

Amesema viashiria vya kitaifa vya deni la taifa linaonyesha bado tunakopesheka lakini kunahitajika mipango madhubuti ya ukusanyaji kodi na kulinda vyanzo vya mapato yasiyo ya kikodi.

“Ni lazima wigo wa walipa kodi uongezeke ili kupata kodi ya kutosha ambayo itasaidia kukuza uchumi wa nchi,” amesema Mutasa.

Amesema pia misamaha ya kodi isiyo na mpangilio ni vema ikafuatiliwa kwa ukaribu ili kuondoa kasoro na kulinda mapato hayo.

Kwa.

upande wake, Mkurugenzi Mtandaji wa TCDD, Hebron Mwakagenda amesema, taasisi hiyo imedhamiria kutoa elimu kwa makundi rika yote ili kuweza kutoa uelewa deni lla taifa na athari za ukopaji usio na tija.

Amesema ipo mifumo mingi ya ukopaji ambapo Serikali imebeba dhamana hata ya kampuni zake zilizokopa halafu zikatoweka.

“Kama kuna hitaji la muhimu la kukopa ni vema ukopaji wake uwe wa tija,” amesema Mwakagenda.

Mwakagenda amesema muongozo wa Afrika wa ukopaji madeni unasisitiza Bunge kuhusika kwenye ukopaji ili kutoa mwenendo mzuri.

Mwakilishi kutoa Chuo Kikuu Mzumbe, Eva Mwambungu alishukuru TCDD kwa kukumbuka kundi la vijana na kuomba kuendelea kujenga uelewa wa ukopaji wenye tija kwa wananchi wake.

Pia, Tunu idd makamu meepnyekiti wa Vijana wa Wafajyakazi wakatoliki Jimho kuu Dar es Salaam