Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mwenyekiti Serikali za mitaa Mafuriko Ilala Bungoni Ally Mshauri amesema wananchi wa Bungoni Mtaa wa Mafuriko wote watampigia kura Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Diwani wao Saady Kimji kutokana na jitihada zao kubwa wametekeleza Ilani kwa vitendo.
Mwenyekiti Ally Shauri, alisema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji mtaa wa Mafuriko Ilala Bungoni wilayani Ilala.
“Viongozi wetu wa Ilala kuanzia Diwani wetu Saady Kimji na Mbunge Mussa Zungu wanafanya kazi kubwa katika kutatua kero za wananchi awali kisima kilifukiwa tukamwambia Diwani wetu Kimji akamwambia Mbunge kisima kikachimbwa tena sasa maji yanatoka mradi mkubwa huu wa jamii “alisema Shauri.
Mwenyekiti Shauri alisema changamoto kubwa ya visima vya maji katika mtaa wa Mafuriko Mbunge Mussa Zungu ametatua ikiwemo shule ya Msingi Kasulu ambapo alisema katika utatuzi wa kero hizo anashirikiana na chama na Serikali.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Ally Shauri alishauri DAWASA ishuke chini kwa wananchi kuchimba visima vya maji safi na Salama.
Wakati huo huo alimuomba Waziri wa Maji Juma Aweso atatue kero wananchi wanaotaka kujiunga na mfumo wa maji taka ambapo alishauri gharama zipungue za kujiunga katika miundombinu hiyo ya DAWASA.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini