Na Heri Shaaban, Timesmajira Online -Dar
Zaidi ya wakazi 7,000, wa mtaa wa Msimbazi Magharibi Kata ya Tabata wilayani Ilala mkoani Dar-es-Salaam,kunufaika na huduma ya mobile kliniki,kufikisha na kutatulIwa kero zao bila kufika kwenye ofisi ya mtaa.
Ambapo wananchi hao watapiga simu kupitia namba maalumu,kwenye ofisi ya mtaa kisha kuwasilisha kero yake ambayo itafanyiwa kazi na Kamati husika.

Akizungumza wakati akizindua huduma hiyo ya mobile kliniki,Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Msimbazi Magharibi,Ramadhan Hamza,lengo la huduma hiyo ni kusikiliza kero za wananchi wa mtaa huo na kutatua changamoto zinazowakabili kwa njia hiyo ya kidigitali.
“Mtaa wangu wa Msimbazi Mangaribi una wakazi zaidi ya 7000 na vikundi vya ulinzi shirikishi viwili,tumeunda kamati ndogo ndogo kwa ajili ya kushirikiana nao,ili tuweze kuisaidia Serikali kutatua kero za wananchi wa mtaa huu,”amesema Hamza.
Hamza ,amesema kuna kero zitatatuliwa na kuishia ngazi ya mtaa,na zitakazo kuwa nje ya uwezo wao wataziwasilisha Kata kwa ajili ya kupelekwa Halmashauri kwa utatuzi zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Msimbazi Magharibi,Harun Adam, amesema katika uzinduzi huo wa mobile kliniki wamechagua kamati kwa ajili ya kupokea na kutatua kero.
Adam, amesema kwa sasa mtaa wa Msimbazi Magharibi vipaumbele vyao ni kutatua kero za mazingira na miundombinu chakavu.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako