Na Zuhura Zukheir, TimesMajira Online, Iringa
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amepitishwa tena na chama chake CHADEMA kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Iringa mjini katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo Msimazi wa Uchaguzi, Fanel Mkisi alimtangaza Mch. Peter Msigwa mshindi kwa kupata kura 117 kati ya 131 zilizopigwa, huku nafasi ya pili akishika Andrew Pallaiga akipata kura 13 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Frank Nyalusi aliyepata kura moja.
Akizungumza baada ya matokeo kutangazwa Mch. Msigwa alisema kuwa anakwenda kupambana na Mbunge wa CCM kwakuwa wananchi wanahitaji kurudishiwa tabasamu lilopotea tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.
Wakati huo huo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum BAWACHA Mkoa wa Iringa, Susan Mgonokulima ametetea kiti chake kwa kuwashinda wenzake watano kwa kupata kura 31 kati ya kura 70 zilizopigwa .
Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo Mgonokulima alisema kuwa ushindi alioupata leo ni wa wanawake wote na anakwenda kuendeleza mapambano ya kuwatetea wanawake.
Aidha aliwataka wajumbe wote kuunganisha nguvu zao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba ili kuhakikisha wanashinda majimbo yote saba na kuitetea Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea