Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online MOSHI
Wakati Bingwa wa Tigo International Kili Half Marathon 2024 aelezea alivyoanza safari yake ya mafanikio kwa kukimbia ‘miguu peku’, Watanzania wang’ara mbio hizo
“Nakumbuka mwaka 2004 nikiwa mwanafunzi wa daraasa la nne katika shule ya Msingi Ligwa iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida nilishiriki Mbio za kilometa tano zilizofanyika Babati Mjinimkoani Manyara nikiwa ‘mguu peku’ na kuibuka kidedea na tangu mwaka huo nikawa na ndoto ya kuwa Mwanariadaha mkubwa nchini Tanzania na ninaishukuru Kampuni ya Tigo kwa kuniwezesha nikaanza kufikia ndoto yangu,” alianza kusimulia Mshindi wa Kwanza wa Mbio Maarufu mataifa za Kilomita 21 maarfufu kama Tigo International Half Marathon 2024, Faraja Lazaro Damas.
Katika Mbio hizo ziliomalizika jana mjini Moshi, Wanariadha wa wa Tanzania wameng’ara kwa kwa kuibuka na ushindi wa kishindo katika Mbio za Kimataifa za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon 2023 zilizofanyika Februari 26, mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) mjini hapa.
Katika hizo, mshindi kwa upande wa wanaume Watanzania wakiongozwa na Faraja Lazaro Damas walishika nafasi tisa kati ya nafasi kumi bora isipokuwa nafasi ya pili iliyoshikwa na Mkenya Peter Mwangi ambapo Damas alitumia muda wa saa 1:03:33 hii y Mwangi aliyetumia muda wa saa 1:03:44.
Akizungumza mara baada ya kuibuka kidedea katika Mbio za Tigo International Half Marathon 2024, Damas kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alimshukuru Mungu kwa ushindi huo pamoja na wadhamini wa mashindano hayo Kampuni ya Tigo kwa kumsaidia kutimiza malengo na ndoto zake za kuwa Mwanariadha mkubwa nchini atakefuzu na kushinda mashindano mbalimbali duniani na kuliletea taifa Medali mbalimbali za Kimataifa.
“Ninamshukuru sana Mungu kwa kipaji alichonijalia kwani kasi ipo kwangu na kasi ipo Tigo 4G na ninaamini kuwa nitakwenda kuiwakilisha Tanzania vyema mwezi Aprili mwaka huu Viena katika kufuzu kushiriki mashindano ya Olympiki yanayotarajiwa kufanyika katika jiji la Paris nchini Ufaransa mwezi Agosti mwaka huu,” alifafanua Damas kwa bashasha.
Kwa upande wa wanawake, Wanaraiadaha wa Taznania pia wameng’ra katika Mbio hizo ambapo Failuna Abdi Matanga aliongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa 1:16:54 akifuatiwa na Mtanzania mwenzake Neema Kisuda aliyeshika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa saa 1:16:54.
Akizungumza katika Mbio hizo, Afisa Mkuu wa Fedha wa kampuni ya Tigo, Innocent Rwetabura alifafanua kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini Mbio za Tigo International Kili Half Marathon(mwaka wa 9 sasa) moja ya mbio za Kilimanjaro International Marathon ambazo zimefikisha miaka 22 yenye mafanikio makubwa.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza waandaji wa mbio hizi kwa kuendesha mbio hizi kwa weledi mkubwa na kuzifanya kuwa za viwango vya kimataifa.” alifafanua afisa huyo na kuongeza kuwa”
“Tangu mwaka 2015, Tigo tumekuwa wadhamini wa mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili International Half Marathon ili kukuza utalii wa michezo, kuibua na kukuza vipaji vya riadha na kuongeza chachu kwenye sekta ya utalii wa ukanda huu wa Kaskazini ikiwemo kuutangaza urithi wetu wa mlima Kilimanjaro.”
Rwetabura aliendelae kufafanua kuwa, Malengo ya Kampuni yaTigo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani tumekuwa na wanariadha wanaoshiriki na kushinda mbio za kimataifa ambao wamekuwa washindi wa Tigo Kili International Marathon.
“Sote ni mashahidi wa ongezeko la wanariadhana utalii wamichezo kwa ujumla na kupelekea mwaka huu wa 2024 kuongeza idadi ya washiriki wa Tigo Kili International Half Marathon kufikia zaidi ya watu 7000” alifafanua CP Rwetabura na kuongeza kuwa;
“Sambamba na hili, Tigo tumeongeza Zawadi za washindi kufikia shilingi milioni 19,420,000/- ili kuvutia wanariadha wengi zaidi kushiriki. Mbali na hapo tumetoa pia zawadi maalum kwa mshindi wa kwanza Mtanzania. Mafanikio haya pia yanaleta hamasa kwenye sekta ya uchumi kwa kuwa mji wa Moshi unahudumia watu wengi hivyo kunufaisha wafanyabiashara na watoa huduma mbali mbali. Mtakubaliana na mimi kuwa, mbio hizi zimekuwa ni chachu ya kuanzishwa kwa mbio nyingine nyingi nchini Tanzania.”
Katika hotuba yake baada ya mashindano hayo Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Damas Ndumbaro aliwapongeza washindi wa mbio hizo ambapo alisema mafanikio yao ymaeakisi matayarisho mazuri waliyoyafanya kabla ya kushiriki kwao.
“Ushindi wenu ni chachu kwa wengine kujiandaa vyema mwakani ili wafanye vizuri na kwenu itakuwa unawapa moyo wa kujituma Zaidi ili kulinda mafanikio mliyoapata”, amesema.
Pia aliwapongeza wandaaji wa mbio hizo kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na chama cha riadha duniani (World Athletics) na kila cha hapa nchini (RT) kwa michango yao iliyochangia Kilimanjaro Marathon iendelee kuwa maarufu.
Aidha aliapongeza wadhamini wengine ambao alisema ni pamoja na kampuni ya Tigo inayodhamini mbio za Km 21 na GEE Sosage mbio za Km 5 maarufu kama Fun Run pamoja na wadhamini wengine ambao ni TPC Sugar, Simba Cement, Kilimanjaro Water, TotalEnergies na watoa huduma rasmi wakimemo Surveyed Plots Company Limited (SPC), GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel na CMC Automobiles na Salsalinero.
Aidha aliwaponheza wadau wengine ambao alisema ni pamoja na Chama Cha Riadha Tanzania, Baraza la Michezo Tanzania, Kamati ya Olympiki, Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU), jogging clubs mbalimbali, Jeshi la Polisi, waratibu wa ndani waandaji Kilimanjaro Marathon Company Ltd, waratibu Executive Solutions na waadishi wa habari.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa