March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MSD yatambua mchango hospitali ya Amana kwa kuipa tuzo

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online-Dar

Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Kanda ya Dar-es- Salaam,imetoa tuzo kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana kwa kutoa huduma bora katika maonesho ya 49 ya Saba Saba.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa MSD Kanda ya Dar-es-Salaam, Betia Kaema, amesema, katika maonesho ya Saba Saba ya mwaka huu,walishirikiana na wauguzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana,kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi.

“Mwaka huu katika maonesho ya 49 ya Saba Saba,tumewahudumia wagonjwa zaidi ya 1200, kwa kushirikiana na hospitali ya Amana.Tunawapa tuzo kwani tumetambua mchango kwa mwaka 2025,”amesema Betia.

Sanjari na hayo Betia, amesema kwa sasa dawa zinapatikana sehemu zote kwa wakati,ambapo MSD Kanda ya Dar-es-Salaam inahudumia Mkoa wa Dar-es-Salaam,Pwani na Morogoro.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt.Mafele Ihoyelo , amesema hospitali hiyo wapo tayari muda wote kutoa huduma ambazo kwa sasa zimekuwa za kisasa.