Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
BOHARI ya Dawa (MSD) imeibuka kinara katika matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) baada ya kutunukiwa Tuzo ya Utendaji Bora katika Ununuzi wa Umma na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
MSD imetambuliwa kama Taasisi Bora kwa Ujumla katika Matumizi ya Mfumo wa NeST kwa mwaka wa fedha 2025/2026, hatua inayoonesha mafanikio yake katika kuimarisha uwazi, ufanisi na matumizi sahihi ya teknolojia katika utekelezaji wa shughuli za ununuzi wa ummaTuzo hiyo ilikabidhiwa Julai 29, 2026, wakati wa Kongamano la 10 la Kitaifa la Ununuzi wa Umma linaloendelea katika Ukumbi wa AICC, mkoani Arusha.
Heshima hiyo inaendelea kuidhihirisha dhamira ya MSD ya kuzingatia misingi ya utawala bora na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kuboresha huduma za ununuzi wa umma.

More Stories
Mhitimu asiyeona aeleza mafanikio ya useremala VETA
JNHPP: Ndoto ya Nyerere yatimia,Rais Samia apongezwa
Rais Samia aagiza wakuu wa Mikoa kujiandaa na udhibiti wa Athari za El Nino