Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa filamu hapa nchini Johari Changula amesema, atawachukulia hatua wale wote waliommzushia kifo kwani si jambo zuri binadamu kumzishia kifo mwenzako huku akiwa hai.
Akiweka wazi hilo kupitia Ukurasa wake wa Instagram huku akiweka picha iliyosema ‘Punzika kwa Amani Msanii Wetu Johari Changula hakika tutakukumbuka’, Johari amesema amesikitishwa sana na kitendo hicho hivyo hana budi wahusia kuwapeleka kwenye vyombo husika.
“Hivi kweli mtu na akili zako unatengeneza ujinga kama huu, hii sasa itakuwa mwisho lazima nichukue hatua .Uhuru wa mitandao mnaitumia kijinga sasa,” amesema Johari kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA