Na Heri Shaaban( Ilala )
MKUU wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo , amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kushusha shilingi bilioni 347 za Maendeleo kwa ajili ya miradi mbalimbali ndani ya wilaya Ilala.
Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, alisema hayo wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya ya kipindi cha Desemba 2024 mpaka February 2025.
“Wilaya ya Ilala Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,ametupatia shilingi bilioni 347 za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya sekta ya Elimu na Miundombinu ya barabara ” alisema Mpogolo.
Mpogolo alisema katika wilaya ya Ilala wanajivunia mafanikio makubwa ikiwemo jitihada za Halmashauri ya jiji katika uongozi wa awamu ya sita ujenzi wa magorofa nane ya shule za Sekondari yapo katika hatua mbalimbali kwa shilingi bilioni 14.4 ambapo pia magorofa kumi yanatarajia kujengwa kwa shilingi bilioni 18 na kuajili walimu 124 wa mkataba .
Aidha alisema kwa upande wa idara ya afya kwa kipindi cha miaka minne idara ya afya inaendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa mujibu wa maelekezo ya Ilani ya chama cha Mapinduzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ibara ya 83 ,utekelezaji huo ni sehemu ya kuboresha miundombinu ya afya ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu chakavu, ujenzi vituo vipya vya afya na ununuzi wa vifaa tiba.
Alisema katika kipindi mafanikio mengine wanayojivunia Ilala kwa upande wa miundombinu barabara za kisasa zinazojengwa kwa kushirikiana na TARURA pamoja na mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP masoko ya kisasa na magari matano wamepokea ya takataka yatakayotumika kubeba taka katika sehemu mbalimbali za Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Pia alisema shilingi milioni 500 wametenga kwa ajili ya vituo vya Polisi na milioni 500 kwa ajili ya CCTV kamera kwa sasa wana mshikamano mkubwa chama cha Mapinduzi CCM na Serikali pamoja na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
More Stories
Wataalam Sekta ya utalii watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu,kujituma na kuwa wabunifu
Shigongo: Rais Samia ameleta mafanikio mengi katika kukuza uchumi
PPRA yatakiwa kuwa mfano kusimamia uadilifu Serikalini