February 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mpembenwe ahoji ujenzi wa barabara ya Bungu-Nyamisati

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

SERIKALI imesema,tayari imeshafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Bungu-Nyamisati katika Jimbo la Kibiti mkoani Pwani.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma Februari 7,2025 na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti Twaha Mpembenwe aliyetaka kujua lini barabara ya Bungu -Nyamisati itajengwa.

“Wapiga kura wa Bungu na Nyamisati wanataka kujua lini barabara ya Bungu- Nyamisati itajengwa ikizingatiwa kwamba upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umeshafanyika.?”amehoji Mpembenwe

Akijibu swali hilo,Mhandisi Kasekenya amesema ” tayari tulishaanza hatua ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ,na nimwombe Mbunge tuonane kwa sababu kipindi hiki ndio tunaandaa mipango kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti inayokuja Ili tuweze kuingiza kwenye mipango ya bajeti ya 2025/26.