December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mpango Kabambe wa Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia waziduliwa

Ni wakusogeza huduma za madaktari karibu na wananchi, ni utekelezaji dhamira yake kuona Watanzania wanapata huduma bora za afya

Na Mwandishi Wetu,Timesmjiraonline,Iringa

DHAMIRA ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya imepata msukumo mpya baada ya kuzinduliwa Mpango Kabambe wa Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia katika hospitali za halmashauri za wilaya nchini.

Mpango huo ulizinduliwa jana mkoani Iringa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, ikiwa ni dhamira ya Rais Samia ni kuona Watanzania wanapata huduma bora za afya.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Waziri Ummy Mpango wa Dkt Samia wa kusogeza zaidi karibu na wananchi huduma za madaktari bingwa ambao kauli mbiu zao ni Madaktari Bingwa wa Dkt Samia, tumekufikia karibu tukuhudumie.

Amesema Mpango huu utafika katika Halmashauri zote 184. Alisema Serikali imeangalia huduma zenye uhitaji zaidi.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, timu ina madaktari bingwa 25, madaktari bingwa wa afya ya uzazi na wanawake, watoto na watoto wachanga, daktari bingwa wa upasuaji, daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, daktari bingwa wa usingizi na ganzi. Wote watafanya kazi za kibingwa kwa siku tano kwa hospitali za mkoani Iringa.

Amesema Mei 13 hadi 17 watakuwa na madaktari bingwa 190 katika hospitali 38 za Kanda ya Kati na Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Rukwa, Songwe na Mbeya.

Mei 20 hadi 24 Madaktari Bingwa wa Rais Samia watakuwa katika Mikoa 3 ambayo ni Dar es Salaam, Pwani na Morogoro itakayojumuisha madaktari bingwa 120 na kutoka huduma katika hospitali za halmashauri.

Mpango huu utaendelea katika hospitali zote ili kupunguza vifo na kupunguza pia mateso ya wagonjwa haswa wale wanaoshindwa kwenda kwenye hospitali za rufaa.

Serikali imejenga majengo ya kisasa pamoja na uwekezaji kwenye vifaa tiba. Mashine ya CT Scan kwa sasa inapatikana katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Hata kwenye Hosptal ya Wilaya ipo mashine ya kisasa ya digital x-ray.

“Zamani watu wenye changamoto za kuugua figo ilikuwa lazima waende Dar es Salaam, lakini leo Serikali imewekeza sana kuongeza wataalam wa afya,” amesema Ummy.

Amesisitiza ubora wa huduma, kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu. “Rais Samia ameandika rekodi duniani na barani Afrika ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kwa asilimia 80.

Kutoka vifo 556 katika kila viazi laki moja hadi vifo 104 katika kila vizazi hai 100.

Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu , akizungmza wakati wa uzinduzi Mpango Kabambe wa Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia . Uzinduzi huo umefanyika mkoani Iringa jana

“Tumsaidie Rais Samia aandike rekodi nyingine duniani ya kupunguza vifo vya watoto vya wachanga kwa sababu hatujafanya vizuri. Vifo vya watoto wachanga vimepungua kwa asilimia 4 tu.

Kutoka vifo 25 katika kila vizazi hai 1000 hadi vifo 24 katika vizazi 1000. Tukiwekeza vizuri kwenye wodi za watoto wachanga tutapunguza vifo vya watoto wachanga hadi asilimia 50,” alisema Ummy.

“Shirika la Afya Duniani linaeleza kwamba tukiwekeza kwenye wodi za watoto wachanga tutapunguza vifo vya watoto wachanga kwa zaidi ya asilimia 50, ndiyo maana tumeanzisha mpango huu kabambe wa madaktari bingwa wa Dkt. Samia ili kuweka msukumu wa kuanzishwa kwa wodi za watoto wachanga ili kuokoa maisha ya watoto wachanga katika hospitali za halmashauri za nchini.

Alisema jambo hilo, sio jambo gumu, linahitaji utashi wa kisiasa, linahitaji usimamizi wa viongozi wote katika ngazi ya mikoa na wilaya.

Amesema wao kama Serikali watanunua vifaa, lakini anatamani vifaa hivyo vipelekwe kwenye ngazi ya vituo vya afya hospitali ya halmashauri hizo kidogo zina mapato.