December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Morocco ya kwanza kufuzu Afcon

Na Mwandishi Wetu. Timesmajira

Timu ya Taifa ya Morocco, imekuwa nchi ya kwanza kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) za 2023, zitakazofanyika nchini Ivory Cost mwaka huu.

Inchi hiyo ilikata tiketi ya kucheza michuano hiyo jana baada ya Afrika Kusini na Liberia kupata sare ya magoli 2-2.

Morocco inaongoza Kundi K, ikiwa na alama sita baada ya kushinda mechi mbili dhidi ya Liberia na Afrika Kusini.

Zimbabwe, ambayo awali ilipangwa Kundi K, iliondolewa na FIFA kucheza mechi za kufuzu AFCON kutokana na serikali ya Zimbabwe kuingilia masuala ya ligi ya soka ya nchi hiyo.