May 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mo Noray amlili Marehemu Mfugale

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MKURUGENZI wa Kampuni ya Tanzania Building Works LTD,

Mohamed Igbal Noray maarufu kama ‘Mo Noray’,amemlilia

aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini

TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale katika kuaga mwili

wake kwenye viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam

leo.

Akizungumza na Timesmajira Online mara baada ya kuuaga

mwili wa marehemu Mfugale Mo Noray amesema,

amesikitika sana kuondokea na mtu muhimu katika Taifa

la Tanzania kutokan na mchango wake mkubwa kwa Taifa.

“Nimesikitika sana kuondokewa na Mhandisi Mfugale,

kwanza alikuwa rafiki yangu kutokana na wote kuwa

wahandisi, alikuwa anajua kazi sana, ki ukweli

tumempoteza Mhandisi mahiri katika taifa letu,”

amesema Mo Noray.

Hata hivyo, amewataka vijana kuiga mfano wake kwa

kusoma kwa bidii ili waweze kuliongoza Taifa kama

alivyokuwa Marehemu Mfugale.