Anaandika Mo Dewji
LEO nimeamua kuanzisha petition (maombi) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa; Uwanja wa Benjamin William Mkapa.
Ujenzi wa Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam ulianzishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ni miongoni mwa viwanja bora katika bara la Afrika kwa sasa.
Uwanja huo kwa namna mmoja au nyingine umesaidia kuendeleza mpira wa miguu na michezo mingine nchini Tanzania. Uzuri na ukubwa wa soka letu umedhihirishwa kwa sababu ya uwanja wetu huo ambao unashika nafasi ya 11 kwa ukubwa Afrika.
Uwanja huo wa kisasa umeongeza uzalendo mkubwa kwa kuwezesha maelfu ya mashabiki kuwa sehemu ya michezo yote mikubwa, pia umeongezea mapato kwa klabu zote na kutuletea heshima kubwa nchini na mifano ipo dhahiri.
Kutokana na uzuri wa uwanja huo, klabu zote za nje ambao huja kucheza katika uwanja huo zimekuwa zikitoa sifa mbalimbali. Timu za mataifa makubwa kama Brazil zimecheza kwenye uwanja huo na kumwaga sifa mbalimbali.
Nje ya michezo, mashindano ya usomaji wa Quran yaliona mkusanyiko mkubwa zaidi kwenye mashindano makubwa ya kusoma Quran barani Afrika, hii nayo ilikuwa ni rekodi nzuri kwetu Watanzania.
Nje ya michezo, mashindano ya usomaji wa Quran yaliona mkusanyiko mkubwa zaidi kwenye mashindano makubwa ya kusoma Quran barani Afrika, hii nayo ilikuwa ni rekodi nzuri kwetu Watanzania.
Tumeshuhudia matamasha mbalimbali makubwa kama matamasha ya Pasaka na Krsimasi yakifanyika hapo na lengo la yote hayo ni kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Itakuwa ni heshima kubwa kama uwanja wetu pendwa utaitwa jina la Uwanja wa Benjamin William Mkapa. Tunamuomba Rais John Pombe Magufuli aridhie kubadili jina la uwanja huo kwa heshima ya Hayati Mkapa ili tuendelee kumkumbuka kwa mchango wake mkubwa na hasa kwa vizazi vijavyo.
Tunawaomba Watanzania wote bila kujali ushabiki wa klabu muunge mkono kwa kuweka sahihi ili tumuombe Rais kubadilisha jina la uwanja huo uitwe Benjamin William Mkapa Stadium au Uwanja wa Benjamin William Mkapa.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati