Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba na Mwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’ ni kama ametoa tahadhari kwa benchi la ufundi la klabu hiyo kufuatia timu hiyo kuolazimisha suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa marudiano wa Ligi Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United kutoka nchini Nigeria.
Amesema ili kuhakikisha wanafikia malengo yao waliyoyaweka msimu huu katika michuano hiyo ya kimataifa basi wanahitaji kujipanga kimbinu na kuzidisha mapambano ili kufanya vema katika mchezo wao wa hatua ya pili ya Ligi Mabingwa dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.
Katika hatua hiyo ya 32 Bora, Simba itaanzia ugenini katika mchezo utakaochewa kati ya Desemba 22 au 23 katika uwanja wa National Sport na kisha watarudiana kati ya Januari 5 au sita katika uwanja wa Mkapa.
Simba imetinga hatua hiyo kwa jumla ya goli 1-0 walilopata katika mchezo wa awali uliochezwa Novemba 29 katika uwanja wa New Jos huku Platinum wakiwafunga Costa do Sol ya Msumbiji jumla ya goli 4-1 baada ya kushinda 2-1 na kisha kushinda goli 2-0 katika mchezo wa marudianoa uliochezwa leo kwenye mji wa Bulawayo.
Akizungumza mara baada ya timu hiyo kutoka suluhu na Plateau katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa na kuvuka hatua hiyo kwa faida ya goli 1-0, Mo amesema kuwa, japokuwa yeye si kocha lakini wanahitaji kufanya mazoezi zaidi ili kuwa bora.
Amesema, katika mchezo huo wamewakosa magoli mengi wapinzani wao lakini pia walipata mipira mingi ya adhabu ikiwemo kona zaidi ya 10 lakini wachezaji wao hawakuweza kutumia nafasi hizo kupata goli.
Amesema, jambo kubwa kwa sasa ni timu yao kufanikiwa kuvuka kwenye raundi ya kwanza
hivyo wanarudi kwenye mikakati na akiwa kama Mwenyekiti atapambana kuhakikisha anapambana na hivyo hivyo kwa wachezaji huku pia akiwataka mashan=biki kuendelea kuiunga mkono timu yao.
Lakini licha ya kufanikiwa kusonga mbele, baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wamemtupia lawma kocha Sven Vandenbrock pamoja na benchi lake la ufundi kwa kushindwa kufanya mabadiliko ya haraka ambayo pengine yangeweza kuwapatia angalau goli moja ili kunogesha furaha yao.
Wamesema, wachezaji si kama walicheza vibaya lakini kuna kitu kilikosekana kwa wachezaji wao hawa safu ya washambuliaji ambao hawakuwa makini kwenye kumalizia pasi za mwisho.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025