Na Esther Macha,TimesMajira Online,Mbeya
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ndele Mwaselela, amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameandika historia kwa kuimarisha sekta ya miundombinu na huduma za afya mkoani Mbeya.
Amedai kuwa kwa mara ya kwanza tangu uhuru, wananchi wa Wilaya ya Mbeya Vijijini wameshuhudia ujenzi wa barabara ya njia nne, mradi uliokuwa ukizungumzwa kwa muda mrefu bila utekelezaji.
“Barabara ya njia nne ilikuwa ni ndoto kwa muda mrefu. Ni Rais Samia pekee aliyeweza kuhakikisha inatekelezwa wananchi wa Mbeya Vijijini Sasa wana historia mpya.
Mwaselela amesema hayo Septemba 8, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na yalizongumzwa na Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dtk.Samia Suluhu alipofanya ziara ya Kampeni mkoani humo mwishoni mwa wiki.
Aidha Mwaselela amesema licha ya mambo mengi yaliyofanywa na Dkt.Samia katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake pia ameweza kuongeza fursa kwa makundi mbalimbali, ikiwemo wanawake, vijana na wafanyabiashara wadogo (machinga), hatua ambayo imeimarisha uchumi wa wananchi wa mkoa huo.
Hata hivyo Mwaselela amesema kuwa wananchi waendelee kumuamini na kumchagua Dkt Samia kwani amedhamiria kuanzisha utaratibu wa kutoa huduma za matibabu bure kwa magonjwa sugu kama vile kisukari, presha na saratani kwa wananchi wasio na uwezo wa kugharamia matibabu.
“Afya bora ndiyo msingi wa maendeleo.Hii ni mara ya kwanza tangu tupate uhuru kwa wananchi kupewa huduma bure za magonjwa sugu. Hakuna utajiri mkubwa duniani kama afya,” amesema.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako