November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mnec Kubecha akitaka Chama cha Act -Wazalendo kuteua vijana makini

Na Mwandishi wetu,Timesmajira,Online

Mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm Nec kupitia vijana Jaffari Kubecha amekitaja chama cha Act Wazalendo kiteue watendaji vijana makini wenye maono, upeo na kufanya upambanuzi katika kujadili na kujibu hoja za kisiasa kwa uyakinifu bila kuingilia mambo ambayo aidha hayajathibitika au kutotolewa hukumu na vyombo vya kisheria vilivyotajwa kikatiba .

Pia amekishauri chama hicho kufahamu kuwa kumzungumzia mtu yeyote au ushauri ambalo bado halijatolewa uamuzi au mtu kutiwa hatiani kisheria ni kosa kumtuhumu mtu, kumnanga mbele ya jamii au kutamja kwa nia ya kumvunjia hadhi, utu au kubaribu heshima yake.

Akito kauli hiyo jana kupitia UVCCM amesema vyama vya upinzani bado vinakabiliwa na tatizo la baadhi ya viongozi wake hususani vijana kuwa na upeo mdogo wa kujua , kupambana na kuielewa dhana ya usimamizi katika mgawanyo wa madaraka na utekelezaji wake.

Kubecha amesema Katibu Halmashauri Kuu Taifa Itikadi na Uenezi wa CCM ,Shaka Hamdu Shaka alijibu hoja iliyotolewa na upinzani unaotaka yafanyike mabadiliko ya kuandikwa katiba mpya na kuachana na ya mwaka 1977 wakati ambao serikali ilioshinda uchaguzi na kuunda dola ikiwa katika juhudi za utekelezaji wa kisera na kutimiza ahadi za kimaendeleo zilizoahidiwa kwa wananchi.

Amesema jawabu la dai hilo limeelezwa kwa ufafanuzi wa kutosha na katibu wa itikadi na uenezi wa Chama chao ambaye alitoa ushahidi jinsi mchakato wa katiba mpya ulivyoanza, kuundwa kwa tume ya kukusanya maoni , uteuzi wa wabunge hadi kuandikwa katiba iliopendelezwa na bunge maalum la katiba na jinsi ambavyo baadhi ya viongozi wa upinzani walivyoukwamisha mchakato huo.

Amesema hata Naibu Katibu mkuu wa Chadema Benson kilagai kitendo chake cha kutoa matamshi yanayoitaka serikali kuwalipa fidia masheikh 36 wa jumuiya ya Uamsho waliokuwa mahabusu kwa miaka minane ni madai yanayokwenda kinyume na dhana ya mgawanyo wa madaraka.

“Kabla hujainuka na kusimama mbele ya kipaza sauti kwanza tafakari unakwenda kusema nini,kwa madhumuni gani na iwapo hutajikwanisha kisheria. Siasa haibatilishi sheria za nchi,”amesema

Kubecha amesema kimsingi katiba iliopo sasa ni katiba bora na makini yenye uwezo na vigezo vinavyojitosheleza kujibu maswali yote magumu unapotokea utata wa kikatiba na kisheria na katiba hiyo haijawahi kushindwa kuelekeza au kutokikidhi viwango vya matakwa ya ufafanuzi kulingana na mahitaji ya wakati.

‘Tumebahatika Tanzania kuwa na katiba ya kizalendo ilioongoza Taifa letu kwa miaka zaidi ya hamsini. Ni katiba iliosimamia na kulinda umoja, utulivu na kujali usawa .Katiba yetu imetuelekeza kila yalipotufika matukio magumu katiba imetulinda ili tusipotee huku ikituonyesha njia sahihi “Amesisitiza Kubecha