KIBAHA
WANANCHI
wanaotumia usafiri wa mabasi ya Mwendo Kasi (DART) kwenye Kiituo Kikuu cha mabasi
Kibaha Mkoani Pwani, (Kibaha Bus Terminal) wametoa malalamiko yao kwa Mkuu Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar
Kunenge ya kwamba inawachukua muda mrefu kupata usafiri huo.
RC
Kunenge alitembelea kituo hicho Mei 2, 2023 katika utaratibu wake wa kawaida wa
kutembelea maeneo yanayotoa huduma za kijamii ili kusikilzia kero au changamoto
zinazojitokeza katika utoaji huduma.
Baada
ya kupokea kero hiyo RC Kunenge alichukua hatua papo hapo kwa kuwasiliana na
uongozi wa juu wa DART ambao nao walimuahidi kuchukua haua za haraka
“Viongozi
wa DART wameahidi kufika kwenye kituo hiki lakini pia kuongeza idadi ya mabasi
yatakayokuwa yakitoa huduma kati ya Kibaha na Dar es Salaam.” Alifafanua.
Aidha
RC Kunenge pia ameelezwa kuwa vibanda vya kujikinga na jua au mvua
havijitoshelezi kwenye kituo hicho hususan kwenye eneo la mabasi ya mwendo kasi
na mabasi madogo ya abiria.
“
Nia ya Mhe Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, na sisi wasaidizi wake ni kusikiliza
na kutatua kero za wananchi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za
kijamii unakuwa rafiki wakati wote.” Aliwahakikishia wasafiri hao.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia alijionea jinsi Kituo hicho kilivyoathiriwa na mvua ambapo kumekuwa
na mashimo.
“Nimewaagiza
wataalma wa Halmshauri washirikiane na TANROADS na TARURA kufanya matengenezo
ya maeneo yaliyoharibika, lakini pia kuhakikisha vikinga jua vinafanyiwa
maboresho haraka.” Alisisitiza RC Kunenge.
More Stories
Mashirikisho yaunga mkono azimio mkutano mkuu CCM
Watumishi wa Mahakama waonywa
CCM ilivyotambua mchango wa wanahabari Mkutano Mkuu Maalum