May 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi Rapha Group aeleza fursa mashindano Tulia Marathoni

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

IMEELEZWA kuwa uwepo wa mashindano ya Tulia Marathoni Jijini Mbeya umekuwa na mwitikio mkubwa kwa jamii na hivyo  manufaa yake kuonekana kwa wajasiliamali ambao wanajishughulisha  na  biashara  mbalimbali za  kujiingizia kipato.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Raphael Group Limited, Raphael Ndelwa mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Tulia Marathoni ambayo yamefanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Ndelwa amesema kwamba mashindano hayo  yamekuwa fursa ya namna ya kukutana wana Mbeya na kuwa kumekuwa hakuna ya kukutana kwenye matukio makubwa ya kuwakusanya na kuwa  kwa eneo moja lakini mashindano hayo yanafanya kuwakutanisha na watu wengi.

“Lakini tukio hili limekuwa likitufanya kukutana na watu wengi wakiwemo wafanyabiashara,wanasiasa,wanamichezo, wafanyakazi hivyo wote tunakuwa tunafanya tukio moja kwa wakati mmoja ,pia naona kuna faida.kubwa katika mashindano haya vijana wetu wanaoshindana wanapata fedha ambazo zinawasaidia kuendesha maisha yao “amesema Mkurugenzi huyo .

Akielezea kuhusu toka kuanzishwa kwa mashindano hayo , Ndelwa amesema kuwa amekuwa akishiriki kila mwaka na mpaka Sasa ni mwaka wa tisa na kwamba kila mwaka yamekuwa yakiendelea kuwa makubwa kuliko yalivyo sasa.

Akizungumzia kuhusu kuboresha mashindano hayo amtaka  wananchi waone kuwa sio ya wageni bali ni ya  wana Mbeya wote  hata kama hawajaweza kuchangia wafike na kujumuika na vikundi mbalimbali ili kukutana na watu wa tofauti”amesema Mkurugenzi huyo.

Kuhusiana na watoto wanaposhirikishwa kwenye mashindano wanaendelea kuwakumbusha wazazi umuhimu wa michezo na wao wataendelea kuwa na kumbukumbu hivyo kitakuwa ni kizazi ambacho kinajengwa kupenda michezo ya namna hiyo,kadri wanavyokuwa wanaweza kufanikiwa na kutoa sapoti.

“Mimi nimeshiriki toka mwaka wa kwanza mpaka sasa mwaka wa tisa kitu kinanifanya nishiriki ni kusikia na kupata kile ninachotaka katika moyo wangu ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali hapa wapo watu kutoka mikoa tofauti tofauti mimi nimejifunza vitu vingi kila ninaposhiriki  kumekuwa na mabadiliko makubwa sanaa ,miaka inayofuata kutakuwa na udhamini mkubwa zaidi ya hapa”amesema Ndelwa.

Fred Mwakibete ni Mbunge wa  Busokelo mkoani Mbeya ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika mashindano hayo amesema  mashindano hayo yameleta fursa  kwa wafanyabiashara kukuza biashara zao .

“Nimefika kushiriki mbio hizi ili kuchangia uboreshaji miundo mbinu ya afya na elimu  Mkoa wa Mbeya kama sehemu ya malengo na ndoto za Dkt.Tulia kuhakikisha eneo la afya na elimu inakuwa na ubora,”amesema.