March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi Penuel Fm achukua fomu kuomba ridhaa kugombea ubunge jimbo la Kibamba

Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dar

MKURUGENZI wa Penuel Fm Radio , Mchungaji Dkt. Alphonce Temba amechukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mchungaji Dkt.Temba amechukua fomu Juni 28,2025 na kukabidhiwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)wilaya ya Ubungo, Masunga Mwenge.