March 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi On Africa Construction ahubiri amani mashindano ya Quran Gongo la Mboto

Na Rose Itono, Timesmajira Online

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Usangu Foundation na On Africa Construction, Niazhan Ibrahim amekabidhi zawadi mbalimbali yakiwepo majiko ya Gesi kwa washindi wa mashindano ya Quran na kuwakumbusha washiriki kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhubiri amani ya nchi

Ibrahim aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza katika mashindano ya tatu ya Quraan yaliyoandaliwa na Taasisi ya Umatul Islamiyya ya Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.

Amesema, mashindano ya Kuhifadhi Quran ni kielelezo cha kuwepo kwa Uhuru wa kuabudu nchini na kusema kuwa anawakabidhi zawadi hizo za mitungi ya Gesi, sabuni za kufulia na vifaa mbalimbali Vya Shule kama mchango wa Taasisi katika kuthamini Quran.

“Mashindano ya Kuhifadhi Quran ni kielelezo cha kuwepo kwa Uhuru wa kuabudu nchini na kwamba Uhuru huo unatokana na upendo baina ya watu wote,” amesema Ibrahim.

Hata hivyo ameisisitiza Jamii hususan waislamu kuendelea kushikamana kwa pamoja bila kujali itiladi za kidini ili kuimarisha umoja na amani ya taifa.

Aidha, amewasihi wazazi na watoto walioshiriki mashindano hayo sambamba na Watanzania wote hususan waislamu kuacha kuchochea vurugu na badala yake Kila mmoja aone umuhimu wa kuhubiri amani

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi iliyoandaa mashindano hayo na mwalimu wa AL Madrasat
Umatul Islamiyya, Abdulaziz Ismaili amesema lengo la kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ilikuwa ni kuwajengea uwezo watoto katika kuisoma dini na Kuhifadhi Quraan.

Amesema, tangu Taasisi hiyo ianze rasmi mwaka 2018, mpaka sasa wamefanikiwa kuwa na jengo lenye ghorofa tatu na tayari wamezindua Madrasa ambayo inafanya vizuri katika kazi ya kuwalea watoto kwenye misingi ya imani.

“Tangu Taasisi yetu ianze rasmi mwaka 2018 hadi 2020 tumefanikiwa kuwa na jengo letu la ghorofa tatu na tumezindua madrasa ambayo mlezi wake ni Alhaji Ibrahim Ismail,” amesema Ismail.

Katibu huyo pia, aliyataja mafanikio ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na Kushirikisha madrasa zingine katika kutoa changamoto kwenye madrasa yao ili kuongeza idadi ya washiriki kila mwaka.

Pia, kufikisha watoto juzuu saba ambao leo hii wameshiriki wa tano Mashindano kujulikana na kutangaza kituo chetu kama kitovu cha elimu na vitendo.

“Taasisi imeweza kifanikisha kujenga msikiti wa kuswalia kwa harambee ndogondogo. Kuanzisha mashindano ya wakina mama juzuu moja na mbili ambao leo wamepatiwa zawadi zao.

Pia. kufanya mikusanyiko ya wakina mama kila ramadhani na matokeo haya ni kuwa na uhusiano ulio mzuri baina ya viongozi na wakina mama hao.

Amesema, Taasisi yao inatarajia kufanya mashindano ya aina hiyo kila mwaka. kuanzisha mfuko wa kujikwamua kiuchumi, kuanzisha mashindano hayo pia kiwilaya ambayo yatapanda hadi kufikia daraja la juu.

Vilevile, kusaidia wasiojiweza mayatima na wajane, kuanzisha program itakayo muwezesha mtoto kujisomea hata akiwa amechelewa madrasa pamoja na kufungua kituo cha watoto yatima ndani ya mwaka huu.

Pia kuanzisha Shule ya awali itakayo mjenga kijana kimaadili na kufikia ngazi ya daraja la kwanza

Hata hivyo alizitaja baadhi ya changamoto za Taasisi hiyo zinazokabiliana ni pamoja na kutopata wadau wa kutosha kuchangia mashindano hali ambayo husababisha kusuasua kwa mashindano.