December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Fyumagwa akabidhiwa rasmi TAWIRI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki amemkabidhi rasmi Dkt. Robert Fyumagwa majukumu ya kuwa Kaimu  Mkurugenzi  Mkuu Taasisi ya Utafiti wa  Wanyamapori  Tanzania- TAWIRI.

Dkt. Robert Fyumagwa anatekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kufuatia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori-TAWIRI, Dkt.Simon Mduma  kustaafu kwa  mujibu wa sheria.

Kupitia hatua hiyo tayari Dkt.Fyumagwa ameanza rasmi kutekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kuanzia tarehe 17 Agosti, 2020.

Akizungumza Jijini Arusha katika Kikao na Menejimenti ya TAWIRI,   Dkt. Nzuki amewataka  watumishi hao  kumpa ushirikiano Dkt. Fyumagwa  katika kutekeleza majukumu yake ikiwa pamoja na  kuimarisha  shughuli za utafiti wa Wanyamapori pamoja na kuendeleza  sekta ya wanyamapori nchini.