March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi INEC aondoa fomu za uteuzi za wagombea kiti cha Rais kwenye ubao wa matangazo

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma

MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Ramadhani Kailima ameondoa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika ubao wa matangazo wa Tume ikiwa zimepita saa 24 za kubandikwa fomu hizo ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria.

Kailima ameondoa fomu hizo jijini hapa leo,Agosti 28 2025 akiongozana watumishi wa Tume hiyo.

Ambapo Fomu hizo za wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilibandikwa ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Fomu hizo zilibandikwa na Tume Saa 10:00 jioni ya Agosti 27, 2025 ambayo ilikuwa ni siku ya uteuzi na kuondolewa leo Agosti 28, 2025 Saa 10: 00 jioni.