December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkubwa Fella ataka Mwijaku akaguliwe Uraia

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MENEJA wa Diamond ambaye pia Diwani wa Kata ya Kilungule, Mbagala Mkubwa Fella, ameitaka Serikali kumkagua Mtangazaji wa kituo cha Clouds Fm Mwijaku, kutokana na Kitendo chake cha kushangilia baada ya Diamond kushindwa kwenye Tuzo za BET.

Akizungumzia hilo kupitia WasafiTV Fella amesemaWatanzania hawana Roho ya Chuki, watu wenye Chuki kama ile wanatakiwa wakaguliwe Uraia wao ili kuwajua kama ni Watanzania au Wakimbizi.

Hata hivyo, Fella amesema ana Kazi nyingine tofauti naya Udiwani na Muziki, na kuweka wazi kuwa anafanya Kazi nyingi sana za Siri alizopewa na Serikali lakini hataki tu kuziweka wazi ili Kulinda amani ya Nchi.

%%%%%%%%%%%%