May 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mke wa Rais wa Msumbiji,Gueta atembelea JKCI

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira

MKE wa Rais wa Msumbiji, Gueta Selemane Chapo amesema anatamani hospitali kama Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iwepo katika nchi yao ukanda wa kusini,kati na kaskazini ili iweze kuwahudumia wakina mama na dada zao.

Aidha, amesema nchi ya Msumbiji itashirikiana na JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili nchi hiyo iwe inatoa huduma za moyo na upandikizaji mimba kama alivyoona wakati ametembelea hospitali hizo.

Gueta amesema hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya katika taasisi ya hiyo jijini Dar es Salaam amesema hospitali ya maputo haiwezi kufanya hayo yote waliyoyaoona katika hospitali hizp, anatamani Msumbiji ije ishirikiane na hizi hospitali kwa huduma za kibingwa.

“Hospitali ya moyo inauwezo mkubwa wa kuhudumia wagonjwa wa nje 2,000 na wanaweza kulaza wagonjwa 100,” Amesema Gueta

Pia, amesema wameona namna wanawake wasioweza kuzaa wanavyosaidiwa hivyo wameweza kujifunza mengi wanatamani wanawake wa nchi yake kupata huduma hizo.

“Tunategemea kutuma ujumbe wetu kuja kujifunza ,tunashukuru sana kwa kuja Tanzania tumejifunza mengi,” Amesema

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dk Peter Kisenge amesema kikubwa alichokuja kuona ni teknolojia ambayo ipo ya kisasa ya kuwafatilia wagonjwa wanapofanyiwa upasuaji wakiwa nyumbani kwa kuwekewa shuka maalum.

Kisenge amesema kupitia shuka hiyo wanaona mapigio yao ya moyo, presha ,upumuaji na mambo mbalimbali kuepusha vifo vya ghafla.

“Ameona watoto waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo na taasisi kwa mwaka inafanya upasuaji wagonjwa 1,000 kwa mwaka na hii ni namba kubwa kwa njia ya tundu dogo wagonjwa 3,000 kwa mwaka na hii ni namba kubwa na sisi ndio wa kwanza Afrika.

Dk Kisenge amesema Msumbiji imeahidi kuendelea kushirikiana nao kwa kuleta wagonjwa na kuleta wataalam wao kuja kujifunza na hiyo ni sehemu ya tiba utalii.

Mkurugenzi wa huduma za tiba,Wizara ya afya Dk Hamad Nyembea amesemalengo la ziara hiyo ni kujifunza huduma zinazotolewa katika hospitali kubwa na Msumbiji wanakuja kujifunza kuona maendeleo makubwa katika huduma za kibobezi.