May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mke wa Achraf apigwa changa la macho

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

Beki wa Kulia wa timu ya Taifa ya Morocco, anayekipiga katika Klabu ya Paris Saint-Germain, Achraf Hakimi hamiliki chochote, licha ya kulipwa fedha nyingi kama mshahara wake kwa mwezi.

Siri hiyo imebainika baada ya mchezaji huyo kufikishwa mahakamani na aliyekuwa mke wake Hiba Abouk aliyeachana naye Machi 27, 2023 ambapo alikuwa akitaka apewe nusu ya mali za aliyekuwa mumewe.

Taarifa kutoka nchini Ufaransa zimeeleza kuwa, baada ya Mahakama kufanya tathimini za Mali za Achraf ilibaini kuwa aliyekuwa mume wake hamiliki chochote kwani mali yake yote imesajiliwa kwa majina ya mamake.

Hakimi anapokea Euro Milioni Moja (zaidi ya Shilingi Bilioni 2.56 kama Mshahara ndani ya PSG kila mwezi lakini 80% (zaidi ya Shilingi Bilioni 1.64) pesa hizo huwekwa kwenye akaunti ya mama yake Bi. Fatima.

“Hana mali, magari, nyumba, vito au hata nguo kwa jina lake.Wakati wowote na akitaka chochote huwa anaulizia kwa mama yake ambaye huwa anamnunulia” Mahakama ilitoa taarifa hiyo.

Inakadiriwa Kuwa Hakimi Achraf ana Utajiri wa Euro Milioni 17 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 45 ila Mali zote zinamilikiwa na Mama yake Bi Fatima.