Na Jackline Martin, TimesMajira Online
KAMPUNI ya Premier Bet, imemtangaza mkazi wa Kongwa mkoani Dodoma, George Leonard Njamasi kuwa amejishindia kiasi Cha shilingi milioni 92, 147, 650 kwa dau la shilingi 500 kwenye mpira wa miguu.
Akizungumza na waandishi wa Habari
Jana Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Eric Kirita amesisitiza
umuhimu wa ustaarabu kwenye michezo hiyo ya kubashiri kwani inapaswa kufanywa kama sehemu ya burudani na siyo chanzo Cha mapato.
“ Ni muhimu kwa wachezaji wote ikiwa ni pamoja na George Leonard Njamasi
kufanya mambo kwa kiasi, kuweka mipaka
na kipaumbele kubashiri kwa ustaarabu”
Kirita amewahimiza wateja wake na jamii ya kitanzania kwa ujumla kutazama michezo ya kubashiri kama sehemu ya burudani, ikiunda mazingira ambayo furaha
inachukua nafasi kuu kuliko faida ya kifedha.
Pia, Kirita amempongeza mshindi huyo kwa kupata ushindi na kumshauri
kuwekeza kwenye ardhi na biashara kwa
uangalifu.
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, Chiku salehe amesema yupo
ajili ya kusimamia na kuthibitisha ushindi
wa George, ambaye amebahatika kupata
ushindi wa shilingi milioni 92, 147, 650.
“Tupo hapa katika kuthibitisha na vile vile
kumshauri George kuwa pesa alizozipata azitumie kwa ajili ya kuendeleza nchi yetu.”
“Niwashauri vijana kuwa, michezo ya kubahatisha sio ajira bali ni sehemu ya burudani wakati unapopata muda
wako wa ziada. Bei ya kubahatisha inaanzia miaka 18 chini ya hapo
watoto hawaruhusiwi kucheza michezo hiyo,” amesema Chiku.
Naye Mshindi wa mchezo wa kubahatisha,
George Njamasi aliwataka wananchi
wote wanaoshiriki mchezo huo, kutokata
tamaa kwani fedha hizo za ushindi zitawasaidia sana kutimiza malengo
yao.
More Stories
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship
Mnzava apania kuwapeleka vijana Simba na Yanga