Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Segerea
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, amesikia kilio cha wananchi wa Kata ya Bonyokwa wilayani Ilala,ambao daraja lao la muda limesombwa na maji yaliosababishwa na mvua za masika na kukata mawasiliano ya barabara Kinyerezi kuelekea Bonyokwa Kimara.
Ambapo katika eneo hilo kuna ujenzi wa daraja la kisasa hivyo ametoa pole kwa wananchi wa maeneo hayo baada ya kivuko cha muda kwenda na maji huku akimpongeza mwananchi aliyerekodi picha mjongeo na kusamba hivyo zikamfikia yeye.

Hivyo amemuagiza Mkandarasi wa daraja hilo kampuni ya Nyaza kujenga daraja la muda haraka kwa ajili ya kuunganisha mawasiliano ya eneo hilo Kinyerezi, Bonyokwa kuelekea Kimara wilayani Ubungo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea miundombinu iliyokumbwa na mafuriko,Bonnah,amesema aliona picha mjongeo(video),ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha daraja la muda katika eneo hilo limosombwa na maji ,hivyo ikamlazimu kufanya ziara ghafla.
.
“Nimekuja kuonana na Mkandarasi aliyekabidhiwa mradi huo pamoja na Meneja wa TANROADS ambao ndio wasimamizi wakuu wa barabara Bonyokwa Kimara.Changamoto mvua inanyesha Kisarawe na Kibaha Mkoa wa Pwani na maji yake yote yanaelekea Jimbo la Segerea hususani Bonde la Mto Msimbazi,”.

Bonnah amesema barabara hiyo pamoja na daraja, ni muhimu kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala na Ubungo,likikamilika litatatua changamoto za usafiri na kukuza uchumi wa maeneo hayo.
Mhandisi wa TANROADS Rajabu Kiamba,amesema jukumu la kutengeza barabara ya muda lipo katika mkataba wa Mkandarasi wa Kampuni hiyo ya Nyanza .
Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya Nyanza,Gribert Bahasha, amesema kwa sasa barabara yac Kimara- Bonyokwa, imefungwa kwa ajili ya usalama wa wananchi pamoja na vyombo vya moto.
“Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo ya Kimara Bonyokwa tulikabidhiwa mwaka 2024 kisha tukaondoa daraja la chuma ili daraja jipya ujezi wake uanze rasmi wakati unaendelea mvua za sasika zimeondoa daraja la muda,”amesema Gribert.

More Stories
Wataalamu wabobezi katika sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi wakutana nchini
Wizara ya afya yachukua hatua sakata la Mzazi anayedai kubadilishiwa Mtoto Arusha
EWURA yatangaza bei za Mafuta kwa mwezi Aprili 2025