January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkali wa mashuti kurejea dimbani

Baada ya kutumia magongo kwa takribani wiki sita, kiungo wa Yanga Mapinduzi Balama anaendelea vizuri sasa akianza kutembea kawaida.

Balama alipata majeraha ya kuteguka mguu katika maandalizi ya mechi za mwisho mwisho kukamilisha msimu uliopitaNyota huyo ameanza mazoezi ya kuutembelea mguu wake uliopata majeraha ikiwa ni hatua nzuri kuelekea kuanza mazoezi kamili

Hii ni habari njema kwa Yanga kwani anaweza kurejea kikosini mapema zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali