March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkadamu aahidi kutatua changamoto za maji Kata ya Milingano

Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online -Tanga

Mgombea Udiwani Kata ya Milingano wilayani Muheza mkoani Tanga,kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mujaheed Mkadamu, Agosti 27,2025 amerudisha fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi hiyo huku akiahidi kushughulikia tatizo sugu la maji.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo, Mkadamu,amesisitiza kuwa endapo atachaguliwa, atahakikisha anashirikiana na wananchi na viongozi wa serikali kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hiyo ya maji pamoja na kuboresha huduma nyingine za kijamii kama elimu, afya na miundombinu.

Mkadamu pia amewashukuru wananchi kwa moyo wa ushirikiano na kuwataka kuendelea kudumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi.