Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini (Mb) amesema kuwa, tayari taratibu zimeanza za ujenzi wa kituo cha Polisi katika Mji mdogo wa Mugeta uliopo Wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Akizungumza katika ziara ya kiserikali ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wilayani Bunda Februari 26, 2024 katika Kijiji cha Mariwanda,Sagini ameeleza kuwa katika mji huo ambao ni maarufu kwa biashara unahitaji kituo cha polisi ambapo Mbunge wa Jimbo hilo Boniphace Getere amekuwa akipigia kelele kwa muda mrefu suala hilo.
“Nikuhakikishie Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kuwa tulipokea ombi la Mbunge kwani kilikuwa kilio chake cha muda mrefu na nikalipeleka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, tukakubaliana kikamilike haraka na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP aliahidi kuwa, mwaka huu tayari katenga fedha kwa ajili ya ujenzi kituo hiki cha Polisi mpaka kukamilika,”amesema Sagini.
Pia Sagini ametoa rai kwa raia kutojihusisha na masuala ya kiuhalifu kwani kufanya hivyo wataendelea kuwa wateja wa Jeshi la Polisi kutokana na jeshi hilo kuongeza nguvu na weledi wa kupambana na vitendo vya kihalifu.
Hata hivyo, ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, inaendelea Mkoani Mara kwa muda wa siku nne ambapo anatembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya zote pamoja na kuhutubia wananchi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi